Naomba mnisamehe ndugu zangu...Hii akili ya 1947 ime-jam!
Hivi kwa mazingira yetu ya sasa ya dot com, ufisadi, ulegelege wa wakulu (Maranya kaita urojo rojo), uzembe, umbeya, kupigana mabao, kungonoka zaidi ya wanyama na kila aina ta ya vituko....kitu gani tunaweza kusema kuwa ni dhambi??
Naona kama huu msamiati sinao tena ingawa walau nachukua uongo (ukiacha ule uongo uliobarikiwa tunaotumia mimi na bibi)!!
Babu DC (1947)
Mkuu mbona umetupa mtihani mkubwa ambao naamini hata wale wanazuoni wa imani ukiwaambia wakuambie dhambi zao watashindwa kutaja...na kuishia kusema vitu ‘generic'.
Na sisi ambao tumeshakata tiketi ya kuwa kuni za motoni ukiuliza dhambi tutakwambia moja tu inayohusu yale yote yanayolenga kuvunja amri ya kutokula tunda la kati bila ruhusa maalumu..
Binafsi naona ziko dhambi nyingi nyingi sana, zilizotajwa na wadau hapo juu ni baadhi tu ambazo jamii imezipitisha..
.Lakini mbona hamtaji zile ambazo ziko lakini jamii haizioni? Kwanini tusitaje zile hisia toka moyoni ambazo zinatusuta daima?
Hebu fikiri unaenda kazini kwenye kagari kako.. uko peke yako unakula kiyoyozi na joto la bongo huku ukiwaacha wengine wamejazana kwenye daladala hata hewa hawana..Hiyo siyo dhambi?." Eti..Moyoni unajisemea wakiangaika kama mimi basi nao watapata usafiri wa kiyoyozi" ....
Wakati wa birthday yako; Christmas, Pasaka, Eid au wakati wa mfungo mtukufu wa Ramadhani..yaani mara moja kwa mwaka ..unaandaa chakula na mapochopocho na kula pamoja na watoto yatima..picha kibao kwenye blog n.k... halafu unawaacha waendelee kufa na njaa kwa siku zilizobaki 364 hadi mwakani..hiyo siyo dhambi?
Unaugua..unalipia ndugu yako pale kwenye hospitali ya ghali. ingawa unashindwa kumwacha ndugu yako afe.. lakini kwa hela ya kumwona dokta tu pale hospitali ya hela ungeweza kutoa huduma ya dawa za malaria kwa kijiji kizima kwa siku 2 kule nyanda za juu..Hiyo siyo dhambi?
Hebu fikiri ..kutokana na mgawo wa umeme..umenunua kagenerator kako..kanapiga kelele mtaa mzima..watoto hawalali..kina mama wajawazito vitoto vinacheza tumboni kwa ajili ya kelele za kagenerator yako.. hiyo siyo dhambi?
Mkuu mimi binafsi huwa nikifikiri na kuona hata nifanye nini nishakuwa kuni za kule Jehanamu kwenye Moto..labda Mola anionee huruma na kuhisi kuni mimi nimelowa na mvua na kunitupa porini ..yaani hata kama sitaenda kwenye pepo nikiwa na zagaa zagaa huko porini mbinguni powa tu…
Kwa upande wa pili nikiachana na fikra za kuwa kuni wa jehamanu .....namuunga mkono LizzY
Nadhani kila ambacho sio haki kumtendea mwenzako/wenzako!!!
Na pia namuunga mkono AshaDii
Dhambi Mzee DC ni relative term... kilicho dhambi kwa huyu sio dhambi kwa yule... hio kutokana na ukweli kua kila jamii ina Imani zake na beliefs zinazowaongoza ni jinsi gani waishi kati ya mtu na mtu au jamii na jamii...
Kimsingi kabisa waweza kuta kila litndwalo hapa duniani ni dhambi kwa mmoja na sio kwa mwingine... hivo kikubwa kwa mwanadamu yeyote it is beta asimamie misingi ya tamaduni zake hasa zile ambazo ni muhimu mno katika kumdefine na pia kuendeleza tamaduni...
Hizo comments mbili za dada zetu hapo juu zaweza kupingana kidogo sana..lakini kwa hali halisi ya hapa duniani..ni sawa tu!