Kitu gani ulidanganywa na Dalali halafu baadae ukagundua ukweli?

Kitu gani ulidanganywa na Dalali halafu baadae ukagundua ukweli?

Mjanja M1

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2018
Posts
4,058
Reaction score
14,382
Madalali kabla ya kukupangisha chumba/nyumba huwa na maneno mengi mazuri ili utoe pesa, maneno mengine huwa ni uongo pia.

Ni jambo gani ulidanganywa na Dalali halafu baadae ukagundua kuwa alikudanganya baada ya kulipa hela ya Kodi?
 
Mimi dalali alijaribu kunidanganya nikamgundua kabla hata hajamalizia uongo wake.

Tulienda kwenye Nyumba Haina Ukuta wa Fensi, nilipomhoji akajaribu kudanganya eti nikilipia tu Kodi, mwenye nyumba atajenga hiyo Fensi.. Swali langu dogo likamshinda Dalali kunishawishi na Biashara ikafia hapo..
 
Kuna nyumba nilipelekwa, baada ya kuicheki nikajaribu kufungua maji yakawa hayatoki. Dalali akasema huwa yanatoka kila siku ni leo tu ndo hayatoki, mwenye nyumba nae akaungana na Dalali kudanganya,..baada ya kuhamia nikashangaa naonyeshwa nyumba ya jirani nikachukue maji, ikawa kila siku naenda kwa jirani kuomba maji hadi mwisho wa Kodi yangu nikahama
 
Zamani Sana maeneo ya Kimara, alinionesha nyumba self na ina mabomba ya maji, akasema Ratiba ya mtaa huo maji yanatoka mara 3 Kwa week, kumbe nyumba haina maji kabisa...yalifungiwa na Dawasco siku nyingi...na choo kinatema!!!!
 
Back
Top Bottom