Kitu gani ulikipenda ukiwa Mtoto

Kucheza kibunduki bunduki.yaani mnaviziana kama magaidi vile ukimkuta mwenzio kazubaa basi unasema "puu puu puu" kisha anaanguka chini na kufa mnaendelea hivyo hivyo hadi timu moja ishinde.ila kuna mijitu inakera yaani unaliuwa alafu halitaki kufa utaskia mi ndo nilikuwahi.

#I miss the life
 
ivi sai uka kutana na miongoni mwao umuulize kwanini alikua hataki kufa kipindikile unadhani itakujibu vipi?
 
iyo xx
 

Attachments

  • 1470340267115.jpg
    7.6 KB · Views: 88
achana na iyo moment apo nimetumwa dukani katika ubora wangu nko na vx rod
 

Attachments

  • 1470340505513.jpg
    23.4 KB · Views: 106
Kupika pika, yani kuanzia kwenye vikopo mpk kwny masufuria, nilikua hodari sana.

Kucheza Rede pia, kama sipo mpira haunogi nitatafutwa au nitasubiriwa mpk nifike.
 
Kucheza sembo(mpira wa karatasi) asubuhi hadi jioni zile mechi za kushindania ndege tuliokua tunawawinda ilikua noma

Kutengeneza magari ya makopo
 
Manati wewe hiyo ndo balaa nilipokuwa nafika Kwa bibi ndege walikuwa wakipataje?
 
Nakumbuka mtaan kwetu kila mchezo una msimu wake na kwa kwel karibia michezo yote niliipenda mfano kampuska,gololi,kutengenez vtu kwa udongo wa mfinyanz...ila kuna mchezo mwingine ulikuwa wa kikatili sana tulikuwa tuna daka vyura kisha tuna wapasua na viwembe tukijifanya n madaktar kwa kwel tuliua vyura wengi sana
 
achana na iyo moment apo nimetumwa dukani katika ubora wangu nko na vx rod
Sasa mie nilikuwa napenda ile ya mfuniko wa ndoo unautoboa kati halafu unakuwa unauendesha na fimbo.
 
Mchezo wangu wa hatari ni kucheza kidali juu ya mti,tena kulikuwa na miti miwili mikubwa ukikimbizwa mti mmoja unahamia mwengine.

Siku mmoja alipodondoka chini na kuvunjika mguu ndipo mchezo tuliacha huo mchezo.
 
Bembea na Gololi nikianza kucheza hiyo michezo hapo kula hadi uje kufuatwa,ili hausikii njaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…