Kitu kilichoipelekea Soviet union hadi ilivyoanguka

Kitu kilichoipelekea Soviet union hadi ilivyoanguka

mchawi wa kusini

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2018
Posts
830
Reaction score
898
Habari Ya muda huu JF Unajua nini kiliiepelekea soviet Union kuanguaka fuatana na mimi.

SOVIET UNION ILIVYOANGUKA- UADUI NA MAREKANI:
Wengi mmesoma au mnakumbuka miaka ile ya vita baridi kati ya USA(Marekani) na Soviet Union(Urusi) na kuletea hali ya kuwa na wasiwasi pengine vita ya 3 ya dunia ingetokea.

Pamoja na kuja kutokea nyufa katika Sovieti Union (ambazo kwa sasa tungeziita expansion joints) CIA au Marekani kwa ujumla walihusika sana katika anguko lililokuja kutokea mwaka 1991 chini ya utawala wa Bush ambaye alikuja kuwa shujaa wa siasa za fitna za nje zilizochezwa kwa umakini sana.

Mara baada ya kuchaguliwa mwezi wa January mwaka 1989 George H.W Bush alitulia na kuangalia namna sasa anaweza kushughulika na sera za mtangulizi wake Ronald Regan katika siasa za nje na hasa suala la vita baridi kati yake na Soviet Union. Bush haraka aliitisha baraza la wataalamu na kuwaagiza kupitia mikakati yote iliyokuwa ikifanyika dhidi ya Soviet Union chini ya Regan. Watu wenye ufahamu wa siasa za kimataifa ,mikakati na Hujuma waliitwa kukaa kujadili mpango mkakati wa kushughulika na Soviet Union pasipo kuingia vitani.

Katika miaka ya 1980 muungano wa Kisovieti ulionekana kuwa na nguvu sana. Ulionesha kuwa umepona kutoka katika jeraha lile la kuivamia Afghanistan. Uchumi wake ulionekana kukua kutoka katika mdumao uliokuwepo karne iliyopita na hapa Soviet Union ikaonekana kuwa na uchumi mzuri kama wa miaka ya 1950s.

Lakini chini chini wakati huo huo kulikuwa na mambo kadhaa yalikuwa yakiendelea katika Muungano huo. Yale maamuzi ambayo yalifanyika kipindi kile cha nyuma ambayo hayakuwa mazuri yalikuwa yameshaanza kujenga nyufa au tuseme yaliacha majeraha kwa baadhi ya washirki wa muungano huo. Kuna mambo kadhaa mbayo nitayaleezea hapa chini kutokana na maelezo mbalimbali ya waandishi na wachambuzi wa siasa hizi za kimataifa.

1. Mipango ya Perestroika na glasnost.

Mikhail Gorbachev alichaguliwa kuwa Rais wa Muungano wa Kisoveit mwaka 1985 (vijana wengi mlikuwa hamjazaliwa miaka hiyo) na alipochaguliwa alikuja na mipango yake miwili kwa ajili ya kuhuisha au kuimarisha nguvu na uchumi wa Soviet Union. Akaja na wazo la Perestroika na Glasnost.

Katika mpango wa perestroika Soviet Union chini ya Gorbachev ilianza kubadilisha uelekeo wake kisisa upande wa uchumi kwa kufanya mchanganyiko wa Ukomunist na Ubepari (kama inavyofanya china sasa) ingawa bado nguvu iliachwa kwa baraza lile kuu ambalo lilifahamika kama Politburo, lilikuwa lina nguvu katika maamuzi na kuelekeza nini kifanyike katika mambo ya kiuchumi.Lakini wakati huo huo serikali ilikuwa na uwezo wa kuruhusu nguvu ya soko kuamua nini kizalishwe kutokana na matakwa ya maendeleo ya Muungano huo. Na hapo kukawa pia na mabadiliko katika uchumi kwa kuruhusu sauti za vijana zisikike kuelekea katika ukuaji wa uchumi mpya. Na mwishone Gorbachev akaanza kuona kuwa kuna uwezekano wa kuwa na uchaguzi wa kidemokrasia kwa chama cha kikomunist kwa ajili ya muungano wa kisoviet.yaani alianza taratibu kulegeza ile misimamo mikali ya itikadi za Kikomunist.

Mpango wa pili wa Gorbachev Glasnost ukaangalia suala la vikwazo mbalimbali kwa wanajamii wa kisovieti. Tukumbuke kwa miaka mingi sana wananchi waliishi bila uhuru wa kujieleza au kueleza mawazo yao. Utawala wa kikomunist huwa ni kama utawala wa mkono wa chuma.Serikali iliongoza kuelekea uelekeo flan na wananchi wanatakiwa kufuata. Hivyo hakukuwa na uhuru wa kujieleza wala uhuru wa dini. Na wengi walikamatwa ikiwa walivunja misingi hii miwili. Lakini Gorbachev alikuja na kuwalegezea mambo haya akiruhusu sasa waweze kujieleza na kuwa huru katika Imani zao.

Mabadiliko haya yalichochea sana kuanza kuanguka kwa Soviet Union badala ya kuimarisha kama ambavyo yeye alikusudia. Na hii ilitokana na utamaduni ambao tayari ulikuwepo katika nchi hizo ukilinganisha na nchi za Kibepari. Serikali ikaanza kuonesha udhaifu wake kwa watu wananchi ambao sasa walikuwa na uwezo wa kuikosoa serikali na kuanza kuunda makundi mbalimbali yenye maono tofauti.

2. Politburo iliyokuwa imezeeka ilianza kujisahau na kujitoa kwenye dhana nzima ya ukomunist.

Tukirudi nyuma miaka ya 1920 usovieti iliyokuwa ikiongozwa na Vladimir Lenin, Leo Trosky na Joseph Stalin. Hawa watu walikuwa na makosa yao. Lakini wao walisimamia hasa dhana ile ambayoMarx aliielezea kuhusiana na Ukomunist ambayo isingekuja kubadilishwa katika kizazi kilichofuata baada yao ili taifa lao liendelee kusimama katika misingi ile ile.

Kuondolewa kwa Nikita Khrushchevmwaka 1963 kulionesha kubadilika kwa misingi mikuu ya siasa cha kisoviet. Huyu ndiye aliyekuwa kiongozi wa mwisho katika Soviet Union ambaye alikuwa akiongoza katika misingi ile halisi ya kimapinduzi. Na kuanzia mwaka 1963 na kuendelea Politburo ikawa inajiondoa mbali Zaidi na Zaidi kutoka katika maono ya Lenin katika masuala mbalimbali. Wakaanza kukengeuka au kuacha misingi ya Kikomunist ya ule ukomunist wa kale.

Miaka ya 1960 mpaka 1970 kulikuwa na ongezeko la utajiri na nguvu kwa viongozi wana ukomunist kindaki ndaki wa chama cha kisovieti (viongozi walijilimbikizia mali). Wale waliokuwa vigogo wa chama. Wananchi wa kisoviet waliliona hili wakiangalia namna gani viongozi wao walikuwa wakitajirika na kuwa na nguvu wakati mamilion ya wananchi wengi wakifa kwa njaa. Baraza la Politburo lilikuwa likijineemesha na kufurahia maisha ya anasa kwa kuwa na magari mazuri kutoka Ujerumani wakila chakula cha gharama, toka Ufaransa na kulalia matandiko mazuri kutoka Italia. Wananchi walikuwa wakiishi katika hali ngumu sana(JITAHIDI USOME ANIMAL FARM ya mwandishi George Orwell). Unafiki wa Politburo ukatengenesha manung’uniko kutoka kwa kizazi kipya ambao waligoma kuendana na mawazo ya chama kama ambavyo wazazi wao pia walianza kukataa chama kushika hatamu. Na kulipofanyika jaribio katika miaka ya 1980s vijana hawa hawakuwa tayari kujitokeza kusimama mbele kuipigania nchi yao. Uzalendo ulikuwa umekufa.

3.Mapambano kutoka nchi za magharibi.

Hata kabla ya utawala wa Jimmy Carter mwaka 1979 USA ilikuwa imechochea vita baridi kwa kiwango kikubwa toka miaka ya 1960 na hata baadaye Ronald Reagan aliingia White House mwaka 1981 kama mpinzani mkubwa wa Soviet Union akiita ni himaya yenye uovu (Evil Empire) na kuweka wazi malengo yake ya kuisambaratisha.

Utawala wa Reagan ulijikita katika kuzalisha silaha kali za kivita kujiandaa kwa lolote lile ikiwa itahitajika kuivamia Soviet Union na kutengeneza Silaha ambazo zilionekana kuwa zingedhoofisha silaha za Wasoviet ikiwa wangejaribu kupambana na USA. Na hili likaweka wazi kuwa kuna ushindi wa wazi kwa marekani ikiwa vingetokea vita.

Reagan hakuishia kwenye Uvumbuzi na matengenezo ya silaha za kivita za kuidhoofisha Soviet Union. Alianza kushambulia pia uchumi wao. Akaitenga Soviet Union na dunia nyingine kiuchumi na kusaidia nchi nyingine kununua mafuta na kuzalisha mafuta kwa bei ya chini kabisa ili wengi wakimbilie kununua mafuta inchi hizo na kuacha kununua mafuta toka Soviet Union ambayo ilikuwa kitegemea sana Mafuta kiuchumi. Kutokana na kukosa mapato katika mafuta basi Soviet ikaanza kujikuta inachechemea.

4. Bunduki na siagi.

Kila uchumi una mipaka yake katika mambo ya ki rasilimali ili kufanya mikakati au mipango ya ukuaji wake. Ikiwa taifa linajikita sana katika kuzalisha silaha na kuwaacha watu pasipo kuwa na bidhaa za kutumia ili waweze kuwa na maisha mazuri linaanza kudhoofisha morali wa watu wake. Na wakati huo huo kama taifa litajikita sana katika kuzalisha bidhaa za matumizi kwa watu wake kunakuwa hakuna rasilimali za kutosha kuweza kukuza uchumi wake kimataifa kwa kuweza kujilinda dhidi ya nguvu kutoka nje. Hivyo kila bidhaa ilipaswa izalishwe kwa uwiano ulio sawa au kwa kiwango stahiki.

Mpango wa miaka mitano wa Stalin ulikuwa kwa kiasi kikubwa umejikita katika kuongeza uzalishaji wa Bidhaa za kuuza nje ya nchi. Soviet ilikuwa ikihitaji kujiimalisha kiviwanda iweze kushindana na nchi nyingine. Bahati mbaya kwa watu wa Soviet Politburo haikubadilisha uelekeo wa kuzalisha Bidhaa za matumizi ya ndani. Ikajikita Zaidi katika kutengeneza au kuzalisha bidhaa ambazo zilikuwa kwa lengo la kuuza nje na silaha za kujilinda Zaidi na kusahau wananchi wake.Miaka ya 1970 na 1980 maisha ya wasoviet yalikuwa magumu sana, na wengi walijikita katika unywaji sana wa pombe kuondoa msongo wa mawazo n.k wananchi walishindwa hata kumudu kuwa na mahitaji muhimu kama nguo au viatu. Tatizo hili la kiuchumi likawa linashusha hadhi ya Muungano wa Kisoviet kuwa ni Taifa kubwa kutokana na watu wengi kuwa na mateso na kuanza kulia kutaka mapinduzi au mabadiliko.

5. Harakati za mataifa husika kutaka utaifa wao.

Kuanguka kwa Soviet Union pia kunaweza kuhusishwa na Muundo wa Muungano huo ul;ivyokuwa. Tukumbuke kuwa Muungano huo ulikuwa na jamhuri zipatazo 15. Katika mataifa hayo kulikuwa na makabila mbalimbali, utamaduni tofaut tofaut ambao pia ulikuwa kwa kias flan hauingiliana na mataifa mengine ndani ya muungano. Wa Russia wao walionekana kama wakiwakandamiza/wababe au kuwaonea mataifa mengine jambo ambalo lilianza kutengeneza hali ya mataifa hayo mengine kutaka kuwa peke yao.

Mwaka 1989 kulianzishwa harakati za utaifa Mashariki mwa Ulaya baada ya mabadiliko ya kiungozi huko Poland na hali hii ikaendelea kukua na kusambaa mpaka Czechoslovakia, Yugoslavia na upande wa ulaya mashariki. Wengi ya waashirika wa Kisoviet wakaanza kujigawa kulingana na asili zao na hili likachochea harakati hiz huko Ukraine, Belarus na hata majimbo ya Baltic. Hizi jamhuri zikaanza kudai kujitenga na kuanza kujiondoa kwenye muungano na hivyo kuanza kudhoofisha serikali kuu. Na mpaka mwaka 1991 muungano wa Kisovieti ulikuwa umeshabomoka.

UHUSIKA WA USA KATIKA KUANGUSHA SOVIET UNION
Kama ambavyo nilidokeza huko juu sababu mbalimbali za kuanguka kwa muungano wa Kisoviet. Washirika wengi wa muungano huu walianza kuchoka na wakilinganisha maendeleo ya nchi zao na nchi nyingine za ulaya na hata Marekani walianza kuona kama wanaishi maisha magumu na yasiyo na future kwao. Hivyo tawala nyingi za kikomunist zikawa zinapinduliwa na hata kupelekea kuvunjwa ukuta wa Berlin mwaka 1989. G.W.Bush alikuwa akiwa support waasi wengi dhidi ya hizi serikali za kikomunist. Sera ya marekani wakati huo ilikuwa ni reactive not pro-active hivyo bush alikuwa kwa umakini sana akiacha haya matukio yajitokee huko kama vile yeye hahusiki moja kwa moja kuepuka misuguano na kutokumungezea hali ngumu ya kisiasa Gorbachev ambaye alionekana kuendana nao kwa namna flan.hivyo hawakutaka kumgutusha au kumpoteza.

Mwaka huo 1989 Bush alikutana na Gorbachev huko Malta mwezi kama huu siku kama hizi (mapema mwezi wa 12) na hapo Bush alizid kumshawish Gorb afanye mabadiliko kuelekea kwenye demokrasia ili aweze kujiweka sawa kiuchumi hasa kwa kuwa naye alikuwa ameshabanwa mbavu kiuchumi toka utawala wa Reagan.

Gorb akaamua kuruhusu mfumo wa kidemokrasia wa vyama vingi na hili lilikuwa wazo la kiufundi toka kwa Bush kwa lengo la kudhoofisha Ukomunist. Uchaguz uliofuatia mwaka 1990 Gorbachev alijikuta akiwa katika mshawasha au njia panda kutokana na msigano toka siasa za ndani. Boris Yeltsin na watu wengi wengine walikuwa wakitaka uelekeo mpya wa kidemokrasia na mabadiliko ya haraka ya kiuchumi wakati wakomunist kindakindaki wakitaka kutupilia mbali muswada huo wa Gorb.

Wakiwa katika mkanganyiko wa waungane na nani katika ya Gorb na Yeltsin utawala wa Bush ukaamua kufanya kazi na Gorbachev kwa sababu waliona kuwa huyu alikuwa reliable. Mwenye kuaminika ukilinganisha na Yeltsin. Waliangalia maamuzi mengi ambayo aliyafanya nyuma yalikuwa pia ni ya manufaa kwao.

Ukafanyika mpango wa kutia saini makubaliano yaliyoitwa START ambapo moja ya makubaliano hayo yalikuwa ni kuondoa majeshi ya Red Army toka Ujerumani mashariki ambayo yalikuwa yakiikalia Ujerumani. Kwa kuondoa majeshi hayo huko inamaana Gorbachev aliamua kuachia kuungana kwa Ujerumani hizo mbili. Tukumbuke zilijitenga na kuwa na Ujerumani Mashariki na Ujerumani Magharib. Na wakati ule Saddam ameivamia Kuwait, USA na viongozi wa kisoviet walishirikiana pamoja kumkemea na kumwondoa.

Lakini ndani ya Usoviet bado changamoto ziliendelea kuwepo ambapo Moscow wakawa wanamshinikiza Gorb abakize nguvu za chama ili kiweze ku control utawala wa kikomunist ulaya ya mashariki.Baada ya kuanguka kwa Ukomunist Ujerumani Mashariki, Majimbo ya Baltic na Caucas wakaanza nao kudai Uhuru kutoka Moscow. January , mwaka 1991 machafuko yakatokea Lithunia na Latvia. Usoviet ikapeleka vifaru kuingilia na kukomesha harakati zao za kujitafutia Uhuru. Jambo ambalo Bush alililaani sana.

Mwaka huo 1991 Utawala wa Bush ukakaa chini tena kuangalia namna gani Utashughulika na utawala wa Kisoviet. Kukawa na mawazo matatu .

i. Utawala uendelee kumuunga mkono Gorbachev kwa kumpa matumaini kuwa itasaidia kuzui kuvunjika kwa muungano wa kisoviet.

ii. Pia wakati huo huo USA ikimsaidia Yeltsin na viongozi wa Jamhuri mbalimbali ili kuwafanya watimize malengo yao ya kutaka muundo mpya au kujitoa katika Muungano huo. Hivyo waliweza kucheza na pande zote mbili kwa umakini sana.

iii. Na wazo la mwisho lilikuwa ni kumsaidia Gorbachev kwa masharti ambayo yangeweza kuendelea kumletea shida kutoka kwa wapinzani wake na wao kutaka mabadiliko ya kiuchumi.

Mapinduzi ambayo hayakufanikiwa August 1991 dhidi ya Gorbachev yalipigilia msumali kuanguka kwa Muungano wa Soviet. Haya yalikuwa yamepangwa na wakomunist kindakindaki ambapo waliishia kupunguza nguvu ya Gorbachev na hivyo yakamsaidia zaidi Yeltsin na harakati zake za kidemokrasia. Bush alilaumu jaribio hilo la Mapinduzi ila ikawa wazi kuwa Gorbachev sasa alikuwa dhaifu. Na hapo akaamua kujiuzulu nafasi yake ya uongozi wa chama cha kikomunist,na badaye muda mfupi chama kikatenganishwa na urais katika muungano wa Kisoviet.Siku chache baada ya jaribio hilo la mapinduzi Ukraine na Belarus wakatangaza Kuwa Huru kutoka Muungano wa Kisoviet. Majimbo ya Baltic ambayo hapo mwanzo yalijitangazia uhuru yakawa yanataka sasa kutambulika kimataifa.

Kutokana na mabadiliko haya ya ghafla utawala wa Bush ukaanza kuangalia kwa ukaribu kusije kuokea balaa la matumizi ya silaha za kinyuklia kutokana na machafuko yaliyoanza kutokea maeneo hayo. Hivyo September 4 mwaka 1991 aliyekuwa katibu wa secretary of state wa USA bwana James Baker alipendekeza kuwe na kanuni 5 muhimu ambazo zitawaongoza USA katika sera zake za siasa za nje kuhusiana na hizi jamhuri mpya.

i. Kuwe na utawala wa kidemokrasia

ii. Kutambua mipaka iliyokuwepo (wasivamie nchi jirani kwa nia ya kujipanua)

iii. Kuunga mkono tawala za kidemokrasia

iv. Kulinda haki za binadamu

v. Kuheshimu sharia za kimataifa

Na kuwa kama Jamhuri hizi mpya au nchi hiz mpya zingefuata taratibu hizo basi USA ingewaunga mkono. Baker akakutana na Gorbachev na Yeltsin katika kusudio la kuwasaidia katika mikakati yao ya kiuchumi na kuandaa fomula ambayo itawasaidia kiuchumi Russia nan chi hizo ambazo zimemeguka. Wakati huo huo kuruhusu mabadiliko ya kisiasa kwa njia ya Amani kabisa. Mwanzoni mwa December Yeltsin na Viongoz wa Ukraine na Belarus walikutana Brest kuunda Ushirikiano wa Nchi huru (CIS) na hapo kuangusha kabisa Muungano wa Kisoviet.

December 25 mwaka 1991 ile bendera ya Nyundo na Nyengo (Sickle) ikashushwa na kubadilishiwa na Bendera ya Russia yenye rangi tatu. Mapema siku hiyo Gorbachev alijiuzulu nafasi yake kama rais wa muungano wa Kisoviet na kumuachia Boris Yeltsin kuwa Rais mpya wa Russia/Urusi mpya na huru. Na watu dunia nzima waliangalia kwa mshangao namna hii ya kubadilishana madaraka kwa njia ya amani kutoka kwenye iliyokuwa jamhuri ya kikomunist katika muungano wa kisoviet na kuwa taifa lenye mitizamo mbalimbali tofaut tofauti.

Kwa kuangusha Soviet Union,utawala wa Bush ukaifanya Russia iwe imara kiuchumi na kuleta amani Urusi,Baltics na majimbo mengine ya iliyokuwa Muungano wa Kisoviet, Bush akatambua Uhuru wa jamhuri nyingine 12 na kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia na Urusi, Ukraine, Belarus, Kazakhstan, Armenia na Kyrgyzstan. Na February mwaka 1992 Baker alitembelea Jamhuri zilizokuwa zimebakia na kuanzisha ushirikiano nazo wa kidiplomasia zikiwemo Uzbekistan, Moldova, Azerbaijan,Turkmenistan na Tajikistan. Vita vya wao kwa wao vilivyotokea Georgia vilizuia isitambulike na kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na USA mpaka May 1992. Yeltsin alikutana na Bush huko Camp David February 1992 na baadaye kumtembelea ikulu rasmi Washington June. Viongoz wa Kazakhstan na Ukraine wakamtembelea Ikulu pia May 1992.

Kumbuka kitu kimoja muhimu; hata baada ya USSR kusambaratika,Urusi baado ni nchi kubwa kuliko zote duniani,yenye nguvu kubwa ya kiuchumi na kijeshi.Vladimir Putin(mwanafunzi wa Boris Yelstin) amepanga kusumbua dunia nzima,tutarajie usumbufu huu kuendelea hadi wakati USA itakapoamua kunyoosha mkono.Chokochoko yote ya Putin ni ya makusudi.

#USPower
 
Kosa lilikuwa kwa Gorbachev kutaka kufanya mageuzi ya kiuchumi na kisiasa kwa wakati mmoja.


Mwenzake mchina alikomaa zaidi na mageuzi ya uchumi pekee.
 
cha kutia moyo gharama zote hizi USA anazomia kudhoofisha nchi zingine ila bado wabishi hawaishi na wanazidi kuzaliwa kila uchwao...zitaendelea kupigwa mpk parapanda lilie
 
Soviet ilikuwa animal farm haswaa mwamba Stalin alikuwa akiingia bungeni wabunge wote ni kusimama na kuanza kupiga makofi wale watatu wa kwanza kuacha kupiga makofi ilikuwa lazima wauliwe.

Hii ilipelekwa siku moja watu nusu saa zima wanapiga makofi ya kushangilia.
 
Back
Top Bottom