HERY HERNHO
Senior Member
- Mar 4, 2022
- 110
- 458
Kugunduliwa kwa chuma kikubwa cha mviringo kinachofanana na mpira wa miguu katika mji wa pwani ya Japan wa Hamamatsu, takriban kilomita 200 kusini magharibi mwa Tokyo, kumezua wimbi kubwa la uvumi.
Mamlaka za mitaa, polisi na kikosi cha mabomu walitumwa kwenye ufukwe wa Enshuhama kuchunguza kitu hicho kisichojulikana.
Wamegundua tu kwamba chuma hicho cha mvirongo hakina lolote ndani yake na hakina tishio lolote, huku wengine wakishuku kuwa inaweza kuwa aina ya boya.
Wenyeji waliovutiwa tayari wamekuja na majina machache ya kuupatia mpira huo kama vile "yai la Godzilla" , "mooring buoy" na kitu cha "anga ya nje".
Ugunduzi kama huo mara chache huibua mashaka katika nyakati za kawaida, lakini umekuja wakati ambapo kuna wasiwasi juu ya vitu visivyojulikana kufuatia kudunguliwa kwa puto linaloshukiwa kuwa la kijasusi la China na Marekani mapema mwezi huu.
Jumatano iliyopita, Japan iliiarifu China kuhusu kutoridhika kwake kutokana na tuhuma za kugundua puto za uchunguzi kwenye anga yake angalau mara tatu tangu 2019.