cabo
JF-Expert Member
- Jun 15, 2016
- 4,756
- 5,250
Siku moja wakati natokea kwenye mishe za hapa na pale pande za kigamboni nikapanda gari la kigamboni kwenda machingacomplex kwenye gari kama unavyoelewa kwenye magari ya machinga complex kuna ulazima wa kuwa na makonda (sio mkuu wa wakuu wa mikoa) wawili kwa watu wanaotoka pande izo au wanao tumia huo usafiri wanaelewa ni kwasababu ya msongamano wa watu wengi konda mmoja anachukua nauli mwingine anapiga debe ...sasa bwana wakati niko kwenye gari tukapita vituo kazaa tukafika kituo kimoja wapo wakapanda watu wawili age 25+ wale jamaa bwana walinifurahisha sana walikuwa ni wacheshi sana na mimi kama kawaida yangu huwa napenda watu wacheshi wakawa na piga stori za hapa na pale kwa jinsi walivyokuwa wanaongea nikajua tu hawa watakuwa ni watu wa pwani pwani katika story zao za ucheshi wakanijumuisha na mimi basi tukawatunatoa dozi ya story za kuchekesha na kukejeli .....[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]hawa jamaa bwana kilichonichekesha na kufanya niandike huu uzi ni mpango wao wakutaka kumtapeli konda anayekusanya hela kwa msaada wa konda mpiga debe wakapanga dili na konda mpiga debe wakati konda anakusanya nauli majamaa wakanyamaza kimya kama walikuwa hawapigi story konda alipowadai nauli wakajifanya ni mabubu plus viziwi huku wakionyesha ishara zote za kibubu kwakutumia mikono na miguno nilicheka kisiri siri kwakuwa na mimi nilikuwa kwenye mpango wao huku konda mpiga debe akiwacheck tu kwa kuiba iba basi konda anayekusanya nauli akaamua andoke zake maana hakuwaelewa alivyoondoka majamaa yakaanza kuongea kama kawaida yakamtoa konds mpiga debe 200 kwakuwafichia siri yao hawakutosheka waaanza tena kupanga mpango mwingine "ngoja tumuonyeshe wakati wakushuka ndio atachanyikiwa kabisa".. gari likafika machinga complex wakati wakushuka wale jamaa wote walipanda wazima kushuka wakajifanya vilema wote [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] kufika mbele wakaanza kutembea kama kawaida