Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Malkia wa Urembo wa Argentina na Puerto Rico wafunga ndoa
Malkia wa Urembo wa Argentina Mariana Varela na Malkia wa urembo wa Puerto Rico Fabiola ValentinImage caption: Malkia wa Urembo wa Argentina Mariana Varela na Malkia wa urembo wa Puerto Rico Fabiola Valentin
Malkia wa zamani wa Urembo kutoka Argentina na Puerto Rico wamewashangaza wengi walipotangaza katika mtandao wa Instagram kwamba walifunga ndoa.
Malkia wa Urembo wa Argentina Mariana Varela na Malkia wa urembo wa Puerto Rico Fabiola Valentin walikutana katika shindano la urembo la Miss Grand International 2020 baada ya wote wawili kuibuka washindi katika mataifa yao mwaka huo.
Baada ya wawili hao kuorodheshwa katika kumi bora katika mashindano hayo nchini Thailand , wamekuwa na uhusiano wao katika mitandao ya kijamii , kulingana na chombo cha habari cha CNN.
Kulingana na jarida la The People Magazine, waliandika katika Instagram siku ya Jumapili kwa lugha ya Kispanish:
‘’Baada ya kuapa kuweka siri uhusiano wetu , tulifungua milango yetukatika siku maalum. 28/10/22 ❤️✨"
Varela mwenye umri wa miaka 26 na Valentin walisambaza vídeo zenye picha za uhusiano wao , jinsi walivyokutana, pete zao za uchumbapamoja na sherehe na marafiki zao.
Kulingana na CNN, wawili hao walifunga ndoa katika mji wa San Juan nchini Puerto Ricotarehe 28 mwezi Oktoba iliopita.
Baadhi ya watu wakiwemo malkia wa urembo waliwatakia heri njema Varela na Valentin.
Abena Akuaba, mwimbaji wa Ghana na mshindi wa shindano la Miss Grand International 2020, aliwashukuru na kuongeza: "MGI ilifanya mkutano mzuri."
