Kituko Serikali ya Kongo DRC: Ina watumishi wenye umri wa miaka 100 ambao hawajastaafu

Kituko Serikali ya Kongo DRC: Ina watumishi wenye umri wa miaka 100 ambao hawajastaafu

tutafikatu

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2011
Posts
3,327
Reaction score
4,624
Hapa Tanzania tunapiga kelele kuhusu ajira. Wengine tunataka umri wa kustaafu upunguzwe. Ukienda Congo DRC utaona vituko. Kuna watumishi wengi wa serikali wenye umri wa miaka 70 na zaidi waliopaswa kustaafu wakiwa na miaka 65. Cha kushangaza kuna zaidi ya watumishi 250 waliofikisha umri wa miaka 100 na kuzidi.

Watumishi wengi wa umma Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hufanya kazi hadi siku zao za kufa zinapofika, wakitegemea kiinua mgongo, kitu ambacho hawapati.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi

Congo wanafanya kazi Serikalini hadi kifo wakisubiri mafao​

Kinshasa, DR Congo (AFP). Wana umri uliozidi miaka 70 na wakati mwingine hata miaka 100. Watumishi wengi wa umma nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hufanya kazi hadi siku zao za mwisho maishani, wakitegemea kinua mgongo na kutambuliwa, vitu ambavyo hawavipati.

"Ningependa serikali imalize ajira yangu kwa heshima," anasema Bayard Kumwimba Dyuba, (84) mwalimu wa shule ya msingi jijini Lubumbashi, mji mkubwa kusini mashariki mwa nchi hiyo kubwa ya Afrika ya kati.

Dyuba ni mtu mfupi mwenye furaha, akiwa na akili ya ujanja, akisumbuliwa na mgongo kupinda na "kusikia kwa matatizo".

"Nilianza kufundisha mwaka 1968, Septemba 9. Ni kazi niliyochagua... sitaki kuiacha," alisema baada ya swali kurudiwa. Anafundisha darasa la wanafunzi 35 wenye umri kati ya miaka 11 na 12. "Lakini niko mwishoni mwa nguvu zangu."

Kwa hiyo, kwanini hastaafu? "Nataka kuondoka," anasema Dyuba. "Lakini si namna hii, bila chochote! Ningepende nipewe nachostahili."

Anakadiria kuwa dola 30,000 za Kimarekani (sawa na zaidi ya Sh64 milioni za Kitanzania) zitatosha kuwa mkono wa kwa heri unaostahili kwa ajili ya kuondoka, na baadaye kufuatiwa na pensheni.

Lakini kwa miaka kadhaa, walimu wengi na wafanyakazi wa utawala wamesahaliwa, licha ya sheria ya mwaka 2016 kueleza kuwa wale waliofikia umri wa miaka 65 au ambao wamefanya kazi kwa miaka 35 wanaweza kustaafu.

"Tumesahaluliwa, kama tumetupwa," anasema Dyuba, ambaye anasema anapata mshahara wa mwezi wa dola 185 za Kimarekani (sawa na zaidi ya Sh370,000 za Kitanzania).

Katika shule nyingine ya msingi iliyo karibu, mwalimu mkuu amefikisha umri wa miaka 78.

Francoise Yumba Mitwele aliingia fani hiyo mwaka 1962. "Ni stadi yangu, napenda kufundisha," anasema, akiwa amevalia nguo ya rangirangi ya mtindo wa Kiafrika.

Kama Dyuba, amechoka lakini anaendelea kufanya kazi akisubiri "donge nono ili aondoke".

Anakadiria fedha hizo ya kumuondoa kufikia dola 25,000 za Kimarekani (sawa na zaidi ya Sh50 milioni za Kitanzania), ambazo zitamtosha kunua nyumba kwa ajili ya watoto wake.

Septemba mwaka jana, Waziri wa Utumishi wa Umma, Jean-Pierre Lihau alikadiria idadi ya wafanyakazi ambao wamefikia umri wa kustaafu kuwa watu 350,000.

"Kati yao 14,000 wamevuka miaka 90, wengine 256 wamefikia miaka 100. Mwenye umri mkubwa kuliko wote ana miaka 110," alisema, akifafanua kuwa anataka waanze kuwaondoa taratibu.

"Ilishasikika awali, kila waziri anasema maneno hayohayo na hakuna kinachotokea," alisema mwanasheria anayepinga, Hubert Tshiswaka, mkurugenzi wa taasisi ya uchunguzi wa haki za binadamu jijini Lubumbashi, ambayo inasimamia kesi ya wafanyakazi wa umma waliofikia umri wa kustaafu.

"Pensheni haiji na wababa na wamama wazee wanafariki kwa njia ambayo si nzuri!" Tshiswaka anakosoa wizi wa fedha za umma na wahusika kutochukuliwa hatua.

Mitwele pia haoni matumaini kwa sababu tangu waziri atoe tamko hilo hakuna kilichofanyika.

Daah Africa imejaa comedy!
84, yupo job, sasa vijana wanaajiriwaje??
 
Hiyo kitu ilishatokea Hata Tanzania wafanyakazi wengi wa halmashauri za miji wengi walikuwa hadi wanakufa Miaka hata 90 bado wako kazini wa vitengo kama vya usafi nk Miaka ys Raisi Mwinyi bado walikuwepo kipindi cha mkapa ndipo waliondolewa payrol
 
Daah Africa imejaa comedy!
84, yupo job, sasa vijana wanaajiriwaje??
Hilo ni kweli kabisa kwa CONGO!!kuna mzee mmoja nilikutana naye pale UVIRA (SUD KIVU), yeye ni afisa misitu mazao, hata kutembea na shida kweli anatembea ameinama mno, lakini ana kagua ma documaaa!!(documents)anaona kukaa nyumbani bila mafao haikubaliki bora aendelee na kazi tu, akikamata mkaa, samaki, ndio mafao yake nyumbani wanakula!!
Kuna mwingine ni afisa uhamiaji hata kama umelipia visa $ 50!!kama umekwenda kufanya biashara ya mazao, labda mchele, kilo 50 ni zake lazima umpe, kama kibali cha kufanya biashara!!na kule hata ulipe kodi ya dola 3000, hupewi risiti na hutasumbuliwa na mtu yoyote!!
 
Siaiei ufurahia sana kufanya kazi kayika nchi za namna hii.
 
HERI MKOLONI ARUDI AFRICA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Congo kuna mama ntilie group tatu yule auzae ugali kwa kuku wa leo, ugali kwa kuku wa jana na yule auzae ugali kwa kuku wa juzi! yaani kuna dhiki ya kufa mtu !
 
Hilo ni kweli kabisa kwa CONGO!!kuna mzee mmoja nilikutana naye pale UVIRA (SUD KIVU), yeye ni afisa misitu mazao, hata kutembea na shida kweli anatembea ameinama mno, lakini ana kagua ma documaaa!!(documents)anaona kukaa nyumbani bila mafao haikubaliki bora aendelee na kazi tu, akikamata mkaa, samaki, ndio mafao yake nyumbani wanakula!!
Kuna mwingine ni afisa uhamiaji hata kama umelipia visa $ 50!!kama umekwenda kufanya biashara ya mazao, labda mchele, kilo 50 ni zake lazima umpe, kama kibali cha kufanya biashara!!na kule hata ulipe kodi ya dola 3000, hupewi risiti na hutasumbuliwa na mtu yoyote!!
Strategy maadam wanajilipa, serikali inajua hawaingii msituni kushika mitutu
 
Back
Top Bottom