Mnyama kadondoka, asili imechukua mali yake, haya wengine tuendelee na maisha,
Mnyama kafa bila Jina, anatambulika kama Jamaa wa Jua Kali
Mnyama, ukiwa mtumwa, utakufa kama rafiki Yako mbwa,
Mnyama, angekuwepo angewaambia, kati yake na mtu ni nani alikuwa wa kwanza Kufa,
Ni mtu, na Kabla ya Kufa madaktari tayari walimkaribisha ndugu yake MTU anaitwa Sababu, Ili waweze kuondoka wote duniani
Nnaambiwa mtu anazima kama Mwanga wa tochi iliyoisha betri, na haendi mbinguni Wala peponi,
Kwaheri mnyama, kwaheri ya kutokuonana, Kwa maana Nami nitakuwa mfu mnyama, na sitokuona Tena,