Kituo cha Afya cha Sabasaba katika Manispaa ya Morogoro, kimezidiwa na wagonjwa wa kuharisha na kutapika
Kituo cha Afya cha Sabasaba katika Manispaa ya Morogoro, kimezidiwa na wagonjwa wa kuharisha na kutapika wenye dalili zote za ugonjwa wa Kipindupindu, ambapo usiku wa kuamkia Julai 16, ITV imekuta wagonjwa 12 wakiwa wametandikiwa magodoro maeneo mbalimbali ikiwemo sakafuni, kwenye mabenchi ya kukalia, sinki za kunawia na kwenye chumba cha daktari.