DOKEZO Kituo cha Afya Mabawe wilayani Ngara kinawatoza fedha wazazi wanaopeleka watoto Kliniki

DOKEZO Kituo cha Afya Mabawe wilayani Ngara kinawatoza fedha wazazi wanaopeleka watoto Kliniki

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Wananchi wa Kata ya Mabawe Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera tunaipongeza Serikali za Jamhuri wa Tanzania chini ya Dkt. Samia Suluhu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jitihada za Maendeleo katika Kata ya Mabawe katika nyanja mbalimbali za Maendeleo hususani katika uboreshaji wa miundombinu ya Maji, Kituo cha Afya na Shule.

Lakini tunasikitika licha cha uboreshaji mkubwa uliofanyika katika kituo cha Afya Mabawe, Kitengo cha Clinic ya watoto wanatoza Fedha kwa wazazi wanaowapeleka watoto clinic Tshs 200/= kwa kila mtoto kinyume na Sera ya Afya ya mama na mtoto.

Hali hii inapelekea baadhi ya wazazi kuacha kuwapeleka clinic watoto kupata huduma, hii sio sawa kwa mustakabali wa Maendeleo wa Taifa letu.

Naomba viongozi wa ngazi ya Wilaya mchukue hatua kwa hali hii.
 
Back
Top Bottom