DOKEZO Kituo cha Afya Mji Tunduma "Serikalini" kinatoza fedha kumuona Daktari, vipimo na dawa kwa Watoto chini ya Miaka mitano

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest

Nimehudumiwa mara mbili katika Kituo cha Afya Halmashauri ya Mji Tunduma maarufu kwa jina "Serikalini" Kata ya Majengo ambapo walilazimisha nitoe gharama za kumuona daktari licha ya kuwa mgonjwa alikuwa ni mtoto mdogo wa miezi 9 tu.

Nililazimika pia kugharamikia vipimo pamoja na dawa ambazo walidai hazipo pale lakini kwa wenye pesa walipewa dawa hizo hizo ambazo mimi niliambiwa hazipo.

Naomba Serikali iingilie kati suala hili kwani ni tofauti na ahadi tunazopewa na Serikali kuwa mama Mjamzito na Watoto watapewa huduma bure katika vituo vyote vya afya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…