Kituo cha kuuliza maswali ya kijinga On Air

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2014
Posts
15,267
Reaction score
29,917
KITUO CHA KUULIZA MASWALI YA KIFALA 1- NA WEWE ULIZA LAKO NA UTAPEWA MAJIBU NA WADAU MBALI MBALI

i. Shilingi 1000/-ni bei gani?- Kisa wa Mbeya

JIBU:Ndugu yangu swali lako zuri sana, uchumi kwa kuwa umepanda na wewe chukua ngazi uufwatie hukohuko maana ukiwa juu alfu ni kama shilingi 900/- lakini ukiwa chini bei ya alfu ni shilingi 600/-

ii. Niko chuoni nasomea unesi, je unadhani nikimaliza shule nitaweza kufanya kazi gani?- Nene wa Kondoa

JIBU: Ukimaliza utakuwa polisi

iii. Je Iringa kubwa kuliko Tanzania?- Magnus wa mafinga

JIBU: Ni wazi wewe ni Mnyalu, ndio Iringa kubwa kuliko Marekani. Angalia kwenye ramani ya Australia utakuta Iringa kaskazini inapakana na Mexico

iv. Je ni kweli binadamu wana miguu miwili?- El Murieti wa Arusha

JIBU: Huo ni uwongo unaoenezwa na wapinzani, tafadhali usidanganyike. Miguu ya kawaida ina binadamu wawili

v. Nimejiangalia kwenye kioo sikujiona, niko wapi?- Chausiku wa Kisarawe

JIBU: Kioo hicho kitakuwa kibovu, si unajua wachina kila kitu wanaleta feki. Kifupi saa hizi uko ahera

vi. Diamond Platnumz ameacha Ubunge wa Chunya?- Fusu wa Kinondoni

JIBU: Diamond ni Mbunge wa kudumu wa bunge la Senegal, aliacha Ubunge wa Chunya kutokana na tatizo la kupatwa kwa jua

vii. Ukichanganya instagram na whatsapp unapata nini?- Stela wa Ostabei

JIBU: Unapata Google, jamani maswali mengi ni ya kitoto mno muwe mnajijibu wenyewe

viii. Nilikuwa macho lakini nikaota nahamia Dodoma, maana yake nini?- Mwanasiasa wa Kagera

JIBU: Maana yake utafungwa kwa wizi wa michango ya serikali za mtaa

ix. Mkanda, mkende , mkindi, mkondo, ….neno gani linafwata?- Msomi- Mabibo Hosteli

JIBU: Inategemea na kiwango chako cha elimu, wengine watasema mkondo wa maji, lakini jibu sahihi ni mkurugenzi

x. Naweza kupiga mswaki na brash ya viatu?- Vanga- Geita

JIBU: Bahati mbaya hukutaja kabila lako, lakini kwa uhakika kabila lenu mtafukuzwa hapa nchini muda si mrefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…