Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kenya imeifungua kwa muda wa wiki nne runinga ya Mt. Kenya TV kwa kukikuka sheria na kanuni za maadili. Mamlaka hiyo imeitoza runinga hiyo faini ya Dola 5,000 za Marekani kwa kupeperusha kipindi cha vibonzo kilichokuwa na maudhui yasiyo na staha.
Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano, Bi. Mercy WanjauImage caption: Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano, Bi. Mercy Wanjau
Akitangaza adhabu hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Kenya Bi. Mercy Wanjau amesema walipokea malalamiko kwamba kituo hicho cha runinga kilipeperusha picha zisizofaa mnamo Aprili 19, 2021, saa nane mchana, kinyume na kanuni za utangazaji.
Mt. Kenya TV inayopeperusha matangazo yake kwa lugha ya Kikuyu, inadaiwa kupeperusha vibonzo vya ngono katika kipindi chake ‘Mucii wa Ciina’ wakati ambapo watoto wengi wako nyumbani.
Hii si mara ya kwanza kwa vyombo vya habari vya Kenya kufungiwa.