Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimezindua Ripoti ya Msaada wa Kisheria-2023

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimezindua Ripoti ya Msaada wa Kisheria-2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) leo, tarehe 20 Agosti 2024, kimezindua Ripoti yake ya Taarifa ya utoaji msaada wa kisheria kwa mwaka 2023.

Uzinduzi wa Ripoti hiyo itaambatana na mjadala, ambapo kati ya wazungumzaji ni Dr. Helen Kijo-Bisimba, Dr.Anna Henga ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, wadau mbalimbali wa Mahakama pamoja na wadau wengine ambao utoa msaada wa kisheria.

Updates.......

Dkt. Anna Henga, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, amefungua kikao hicho kwa kusema, “Kwa mwaka 2023, Kituo kilishuhudia mafanikio makubwa katika huduma hizo. Kituo kiliweza kufikia wateja 29,491, ambao ni nyongeza ya wateja 11,197 kutoka mwaka 2022. Hata hivyo, wanawake wameendelea kuwa wachache zaidi ukilinganisha na wateja wa kiume, huku asilimia zikiwa 65% kwa wanaume na 35% kwa wanawake.”

Dr. Helen Kijo-Bisimba
Wasaidizi wa Kisheria wanawafundisha watu kujuwa haki zao na kuwasaidia watu kupata haki zao. Misaada ya Kisheria ni muhimu sana kwa sababu bila hivyo watu wengi watapata shida sana hasa hawa ambao hawana uwezo wa kutoa fedha kwa Mawakili.

Wakili Msomi Fulgence Massawe
Ameleza kutoa Ripoti ya msaada wa Sheria walioifanya mwaka 2023.

Wakili Msomi Fulgence Masawe ameeleza Umri wenye migogoro mingi zaidi ya Ardhi ni miaka 45 hadi 54. Katika kesi za ardhi 66% ni Wanaume lakini Wanawake wamekuwa wakijitokeza zaidi kwenye migogoro ya kifamilia.

Aidha matatizo mengine yanayo tokea kwenye ngazi ya familia ni Mirathi lakini Talaka inaongoza kwahiyo kwa kweli Talaka zinaongezeka kwa kasi sana. Wanawake wanapeleka mashauri mengi sana kwa ngazi ya familia.

Kwa upande wa ajira Wakili Msomi Fulgence Masawe amesema migogoro mingi ya ajira ni kuachishwa kazi, uvinjifu wa mikataba, social security.

Kwa mwaka 2023 wateja 7245 walijengewa uwezo kusimamia mashauri yao wenyewe, lakini 1224 waliwakilishwa Mahakamani.

Dkt. Anna Henga, Mkurugenzi Mtendaji LHRC​

“Aidha, makosa mengi yalirekodiwa kuwa ya kujamiiana, hususani ubakaji na ulawiti, na mengine ni wizi wa kutumia silaha, madawa, na utakatishaji fedha. Kwa watoto wanaokinzana na sheria, kituo kimeshuhudia asilimia 95 ya watoto hawa wakiwa wa kiume na asilimia 5 wa kike, huku wengi wao wakishtakiwa kwa makosa ya kujamiiana na wizi. Hii inatupa tathmini kuwa bado jamii, hususani watoto, wapo katika hatari kubwa ya kufanyiwa ukatili, hususan wa kingono. Aidha, hali ya maisha inayoendelea kupanda inafanya watu kushindwa kumudu majukumu ya kila siku, hivyo kujikuta kwenye mikono ya sheria.”

FB_IMG_1724135785756.jpg


View: https://www.youtube.com/live/5z77LWIiOxo
 
Back
Top Bottom