Kituo cha Uwekezaji chakamilisha ujenzi wa Mfumo wa Kielektroniki wa Kuhudumia Wawekezaji (TeIW) awamu ya kwanza

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Katika Mwaka 2023/24, Kituo cha Uwekezaji kimekamilisha ujenzi wa Mfumo wa Kielektroniki wa Kuhudumia Wawekezaji (Tanzania Electronic Investment Window - TeIW) kwa awamu ya kwanza ambao ulizinduliwa Septemba, 2023

Mfumo huo umeunganishwa na mifumo ya Taasisi saba (7) ambazo ni Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya Uhamiaji, Idara ya Kazi, Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na TIC.
Mfumo huo, unamuwezesha mwekezaji kusajili mradi popote ndani na nje ya nchi na kupata vibali vya uwekezaji ndani ya siku 3 ikiwa ametimiza vigezo.

Awamu ya pili ya ujenzi wa mfumo huo itahusisha uunganishaji wa Taasisi nyingine saba (7) ambazo ni Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Wizara ya Kilimo, Tume ya Madini na Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA).

Soma Pia: Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kinara Tuzo ya Taasisi Bora ya Uwekezaji Afrika

Chanzo: Jamhuri Media
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…