KITUO KINACHOFATA NI POSTA YA ZAMANI

KITUO KINACHOFATA NI POSTA YA ZAMANI

Uta Uta

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2016
Posts
3,740
Reaction score
8,751
Jana katika pirika pirika zangu za kuzunguka jiji la Dsm nikiwa natokea feri, kuna kituko kilitokea kikamuacha kila mtu mdomo wazi na minong'ono ya hapa na pale. Kuna kijana mmmojaa ambaye jina lake halikuweza kupatikana na haikujulikana anaelekea wapi akiwa na umri wa kati ya miaka 25 na 30 hivi,alikuwa anaongea na simu tukiwa maeneo ya Mahakama kuu huku ikionekana akimlaumu mwenzake kwa kutojali mda, sasa kimbembe kikaja kwa huyo jamaa baada ya mwenzake kumuuuliza wewe uko wapi, jamaa kwa kujiamini akasema ona sasa mi nishafika Magomeni we bado hata hujatoka, mungu si Athumani mara hizi gali zenu za mwendo kasi tena si unajua tena king,ora kikalia "kituo kinachofuata ni posta ya zamani" sasa jamaa akaulizwa unasema uko wapi ikabidi jamaa ageuke kushoto kulia kisha akakata simu bila kutoa jibu lolote na akiwaacha abiria hoi kwa kicheko. Tuwe makini tukiwa katika haya mabasi na zile alarm zao usije mzee ukaumbuka ikawa msala. Nawatakia ijumaa kuu njema, ntarudi kikjijini mda si mrefu naogopa nisije kumpa mtu mimba mjini hapa ikawa balaa
 
We hudhani stress za maisha zilizosababishwa na CCM hazina mchango kwenye upungufu wa nguvu za kiume!?
Kwahio wewe unadhani kuna mtu au chama kitakuondolea stress zako? Pambana kijana wewe ndio unaeweza kujikwamua hakuna wa kukutoa hapo ulipo.
 
Back
Top Bottom