Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
KITWANA ZANGIRA (ZINGARO) WA BIBI MAMA KITWANA WA MTAA WA MCHIKICHI
Hii picha hapo chini inamuonyesha Mwalimu Nyerere ni kutoka katika clip ya documentary ya Bibi Titi.
Kulia ni Kitwana Zangira lakini huyu si yule ambae wengi walimfahamu kwa kesi ya ujasusi.
Kitwana huyu ni mwingine.
Mama yake Kitwana huyu mimi nikimwita Bibi Mama Kitwana.
Mama Kitwana alikuwa na udugu na ukoo wetu lakini sijui kwa vipi.
Nyumba ya Mama Kitwana ilikuwa Mtaa wa Mchikichi karibu na Dar es Salaam Jazz Band.
Mara nyingi nikiwa na baba yangu Kariakoo katika utoto wangu tulikuwa tukienda nyumbani kwake kumwamkia.
Mwanae Kitwana kumbukumbu yangu ni kumuona ndani ya Land Rover ya TANU.
Kwangu mimi Kitwana Zangira alikuwa kaka mkubwa au baba mdogo kwani yeye alikuwa mdogo kwa baba yangu.
Alikuwa kijana mtanashati.
Nilikuja kujua kuwa alikuwa TANU Intelligence miaka mingi baadae nilipopata akili ya utambuzi wa mambo.
Nakumbuka mwaka wa 1964 niko Tabora kwa babu yangu Salum Abdallah kiongozi wa Tanganyika Railways African Union (TRAU), Kitwana Zangira alikuja nyumbani na Land Rover ya TANU kaongozana na wenzake.
Wakati huu babu alikuwa katiwa kizuizini Jela ya Uyui kufuatia maasi ya Tanganyika Rifles (TR) tarehe 20 January 1964.
Kuanzia hapa sikumsikia tena Kitwana Zangira wala mama yake, Mama Kitwana.
Kiasi cha miaka 10 iliyopita nilimuona Kitwana Zangira sasa kazeeka na kachoka yuko kakaa kituo cha basi
Magomeni Mapipa anasuburi usafiri.
Waingereza wanasema, "A shadow of himself."
Si Kitwana yule wa miaka ya 1960 wa sura jamil na mtanashati.
Kwa kumwangalia nilijua ni mgonjwa na dunia imempiga.
Juu ya hali yake alionyesha furaha kuniona.
Tukazungumza kwa muda mfupi tukaagana.
Kitwana wa Mama Kitwana sasa ni marehemu.
Mimi na Kitwana Zangira sote tuko katika documentary hii ya Bibi Titi na sote tumeyaona yaliyopita katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika kwa macho yetu ingawa yeye alikuwa mkubwa na yuko ndani ya TANU kama kachero.
Kitwana Zangira wa Bibi Mama Kitwana alikuwa mmoja wa vijana waliokuwa walinzi wa Julius Nyerere.
NB
Nimefahamishwa na Iddi Chaurembo kuwa jina lake hasa ni ''Zingaro.''
Iddi Chaurembo ni mkubwa kwangu kwa umri.