Kiuelewa na kujitambua binadamu wapo aina nne

Kiuelewa na kujitambua binadamu wapo aina nne

Tyrone Kaijage

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2021
Posts
1,617
Reaction score
3,405
1. Mtu anayejua, na anajua kwamba anajua. Huyu ndiye mwanazuoni, basi mzingatieni na mjifunze kwake.

2. Mtu anayejua, lakini hajui kwamba anajua. Huyu amesahau, basi mkumbushe kimya kimya.

3. Mtu ambaye hajui, na anajua kwamba hajui. Huyu ni mwanafunzi basi msomeshe mfululizo maana siku moja atakuwa mwanazuoni au msomi mkubwa.

4. Mtu ambaye hajui, na hajui kwamba hajui na hata hajali kujua. Huyu ni mjinga, basi mkatae.

IMG_6339.jpg
 
Mimi huwa napenda kimujifunza kila siku kutoka kwa watu walionizid maarifa

Hila watu wengi hawapendi kujifunza kukosolewa na wataka kubaki nacho kile wanachokijua wao
 
ujatuonesha hizo namba na watu ulio waweka
 
Na kuna wale ambao hawajui ila wanajifanya wanajua. Hata wakiwa kwenye kadamnasi atataka kila mtu ajue kuwa yeye anajua wakati hajui. Na hajui kama hapo kuna watu waliomzidi elimu na maarifa ila anawaona wote wako chini yake kwasababu hajui kama yeye ni zwazwa.
 
Unaposema mtu anajua una maanisha kujua kitu gani?

Coz hakuna Binadamu anayejua kila kitu,utofauti wetu wa kujua au kutambua vitu tofauti tofauti ndio umeifanya Dunia ya leo kua hivi,hatuwezi kujua jambo moja watu wote,

Kila Binadamu ana umuhimu wake kwenye sehemu yake na kwa anachokijua ambacho kinakua na impact nzuri kwenye jamii.
 
1. Mtu anayejua, na anajua kwamba anajua. Huyu ndiye mwanazuoni, basi mzingatieni na mjifunze kwake.

2. Mtu anayejua, lakini hajui kwamba anajua. Huyu amesahau, basi mkumbushe kimya kimya.

3. Mtu ambaye hajui, na anajua kwamba hajui. Huyu ni mwanafunzi basi msomeshe mfululizo maana siku moja atakuwa mwanazuoni au msomi mkubwa.

4. Mtu ambaye hajui, na hajui kwamba hajui na hata hajali kujua. Huyu ni mjinga, basi mkatae.

View attachment 2483068

Mkuu hup sahihi kuna watu hawajui lakini hawataki kujifunza na zaidi wanashikilia kile wanacho kiamini kwamba ni sahihi hiliali sio sahihi

Hawa tuna waweka kundi la denial in psychology ambo mtu hanakataa ukweli hili hali anajua ukweli na anafanya hivyo for the purporse to feel good
 
Back
Top Bottom