Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Taasisi ya Twaweza leo Mei 07, 2022 inawasilisha Matokeo ya mbinu ya motisha ya KiuFunza Jijini Dodoma.
KiuFunza ni Mpango unaotoa bakshishi kwa Walimu kulingana na matokeo ya ujifunzaji wa Wanafunzi. Mpango huu umefanyiwa majaribio tangu 2013.
KiuFunza ni Mfumo wa Motisha unaounganisha malipo ya bonasi ya Walimu na ujuzi wa KKK (Kusoma, Kuandika na Kuhesabu) unaofanywa na Wanafunzi wao
Majaribio yaliyofanywa na Taasisi ya Twaweza kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu pamoja na Ofisi ya Rais - TAMISEMI yameonesha Malipo ya Fedha kwa Walimu kulingana na utendaji yanaweza kuchangia kuboresha Stadi za Msingi za kusoma/kuhesabu kwa Wanafunzi wote wa Elimu Msingi
KiuFunza na tafiti nyingine zinaonesha motisha ya Walimu, Uwajibikaji na jitihada za kusaidia Wanafunzi wafanye vizuri zaidi ni nadra sana
Ushahidi kutoka duniani kote unaonesha kuwa jitihada za Walimu zina mchango mkubwa kwenye kuboresha matokeo ya kujifunza
====
Updates
Twaweza: Ni 17% tu ya Walimu ndio wanaopenda kufundisha Madarasa ya Mwanzo ya Shule za Msingi (Darasa la I-III)
Hii inamaanisha Walimu hawana ari ya kufundisha Madarasa haya Muhimu
Mazingira ya kufundishia na kujifunzia ni magumu zaidi kwa Madarasa ya mwanzo
PROF. MKENDA: TUMEANZA MCHAKATO WA MAGEUZI MAKUBWA YA ELIMU
Akizungumza leo Mei 7, 2022 wakati Twaweza ikiwasilisha Matokeo ya #KiuFunza Jijini Dodoma Waziri wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda amesema, "Kuna masuala 7 tunayaangalia ambayo ni Sera, Sheria ya 1978, Mitaala, Idadi ya Walimu na Wakufunzi, Ubora wa Walimu na Miundombinu"
PROF. KITILA MKUMBO: LAZIMA TUWAPIGANIE WALIMU
Mbunge wa Jimbo la Ubungo ambaye pia ni Mdau mkubwa wa Masuala ya Elimu, Prof. Kitila Mkumbo amehoji ni kwanini inashindikana kuwapa Motisha Walimu?
Amesema Motisha ina umuhimu mkubwa na Walimu lazima wapiganiwe
Aidan Eyakuze: Mwalimu anastahili kuheshimiwa na kuthaminiwa. Wote tunafahamu Jamii iliyostaarabika ni kwasababu ya Walimu
Twaweza tumetoa mfano huu wa KiuFunza, tumewekeza katika kuonesha Motisha inafanya kazi kwenye kuhakikisha Watoto wanapata stadi za Msingi
MKURUGENZI HAKIELIMU: TUTAONA MABADILIKO MAKUBWA TUKITHAMINI WALIMU
Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, Dkt. John Kalage ametoa rai ya Walimu kuthaminiwa, akisema wanachofanya kikipewa thamani, Tanzania itashuhudia Mabadiliko makubwa kwenye Elimu
Amesema japo Ualimu ni Wito, ni lazima Mwalimu aone kama anachokifanya kinathaminika na kuheshimika