Kiukweli huyu mchezaji wa soka zamani Alphonce Modest anahitaji msaada

Ugonjwa ni kitu kibaya sana dakika 5 ushakiwa masikini.

Waweke utaratibu watu watachangia, wale mashabiki 60,000 wanaojazaga uwanja wa taifa wakitoa hata 500 kila mtu hiyo ni milini 30 tayari itamsaidia sana
 
Niwe mkweli nimeumia sana lakini mbele ya Mungu na sisi wapenda soka tukiungana kila kitu kinawezekana.

Bonge moja la beki miaka hiyo kwa sisi wakongwe. Watanzania ni watu waungwana sana tunaweza kumchangia pesa za matumizi na hata matibabu. Unaweza kukuta jamaa amelala kitandani kumbe ugonjwa wake unatibika hasa ukuzingatia mbinu mpya za matibabu zinagundulika kila siku. Na familia ya wapenda mpira sijui tuna nini tunashindwa hata na familia ya tweeter siku hizi inaitwa X. Kule ishu kama hii tokea muda uzi ulipowekwa mpaka sasa hivi ungekuta watu washajitolea zaidi ya hata milioni 50.

Ombi langu kwa Simba, Yanga na TFF ajitokeze mtu trusted kati yenu tupeni namba ya simu na benki akaunti tuanze kutupia pesa huko kidogo kidogo kama wanavyofanya wanafanilia X. Kwa michango na imani ya mwenyezi Mungu tunaweza kumsaidia Alphonce Modest akasimama tena hata kama sio kimwili basi hata kiuchumi na tukamrdishia angalau tabasamu lake na tumaini jipya.

Amina
 
Mungu amsaidie
 
Modest anaanza, kufunguka kwa kusema ukweli nyie wanawake ni wanyama sana, mliokosa huruma na utu.
Pengine mwanamke ndio chanzo cha matatizo yake.

Pole yake waweke taratibu nzuri watu wachangie atibiwe.
 
Naungana nawewe nitatoka chochote kitu nilicho nacho asee. Zaidi ya yote michango yetu isipite Kwa mangungu
 
Pengine mwanamke ndio chanzo cha matatizo yake.

Pole yake waweke taratibu nzuri watu wachangie atibiwe.
Wenye jukumu la kupaza sauti ni wana michezo wa zamani ambao wengi kwa sasa hawapo katika media wengine ni Mareham mfano

Kina sweedy mwinyi Mareham
Juma nkamia ayupo kwenye media

Haya kina charse hilali hawa wanajua uwezo wa alichokifanya alphonce modest wanaweza semea jambo

Au haji manara anaweza semea hili suala
 
Tukiwa bado na nguvu zetu na utimamu wetu kimwili tujitahidi sana kuwapenda na kuwatendea mema tunaoishi nao majumbani mwetu eg wake zetu baba zetu mama zetu dada kaka wadogo zetu maana hawa ndiyo watakaotufaa wakati wa dhiki kuu.

Nimesoma nikaona jinsi baba yake na wadogo zake wengine wanavyojaribu kumjali ktk wakati huu mgumu kwake nimefarijika sana,mara nyingi sisi marafiki tuliokuwa tunakaa tunakula na kunywa vizuri wakati kama huu tutakujulia hali week mbili za mwanzo wa maradhi yako ikija kugonga miezi sita hata simu tena hatupigi lakini ndugu kwa miaka 14 wapo bega kwa bega na mgonjwa wao hakuna aliyemchoka.

Mungu amponye,sijamalizia kuisoma habari yote may be wameweka namba namba page iliyofuata ningeweka cent kidogo hata ya panadol.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…