Kiukweli Siitendei Haki Fremu Yangu..Msaada.!!

one cater

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2014
Posts
368
Reaction score
153
Habari Za Mchana Wana Jamvi,

Kwa Kifupi Tu Mimi Ni Mkazi Wa Mbezi-Msuguri, Miez 3 Imepita Toka Nilipoamua Kufunga Ofisi Yangu Ya Biashara Ya Uwakala (M-pesa na Tigo pesa).

Kilichonisababisha Nije Humu Ni Kuomba Msaada Wa Mawazo Baada Ya Kufikiria Sana Cha Kufanya Na Kutokupata Jibu La Kuridhisha, Ni Hivi Hapa Ninapofanya Hii Kazi Yangu Kwa Bahati Nzuri Nilibahatika Kupata Fremu Ambayo Ni Kubwa na Kama Mnavyojua Kuwa Hii Kazi Haitaji Eneo Kubwa Sana, Inahitaji Meza Pesa Na Simu Zako Za Kazi.

Sasa Kinachoniumiza Roho Ni Kuona Nimekaa Katika Chumba Kikubwa Ambacho Kipo Wazi Wakati Ninaweza Nikaongeza Vitu Vingine Ambavyo Vinaweza Kuboresha Kipato
Changu.

Nilikuwa Nahitaji Kuongeza Bizness Ambayo Ni Tofauti Kidogo Na Wafanya Biashara Wengi Wa Eneo Hili Nilipo, Maana Hapa Kuna Wafanyabiashara Wengi Kidogo Wa Maduka Ya Rejareja, Vinyawi, Stationary, Japo Nafanya Na Biashara Kama Ya Kuuza Vocha, Kusajili, Tigo Rusha Vyote Nafanya, Ila Sijaridhika kwasababu Bado Nina Eneo Kubwa Lililo Wazi.

Nilichokuwa Nahitaji Ni Idea Nyingine Nzuri Ya Biashara Ambayo Naweza Kufanya Ya Tofauti Kidogo Na Wafanyabiashara Wa Eneo Hili Ambayo Itanisaidia Kuboresha Kipato Changu.

Nimeamua Kilileta Swala Hili Humu kwasababu naamini Hakuna Sehemu Nyingine Ambayo Ninaweza Nikapata Mawazo Mazuri Kama Humu JF.

Nawasilisha.
 
Weka nguo za aina mbali mbali za dukani na mtumba ujaribu kama zitatoka.....
 
Mtaji wako kwanza ni shilingi ngapi?Tusije tukaanza kutiririka kumbe hata kwenye hiyo tigo pesa na Mpesa mtu akija kutoa laki moja unasema hela kwenye account hamna
 

Kwa nini usifikirie Kupanua hiyo biashara yako? mi kwa mtazamo wangu hiyo biashara inalipa sana sema watu wengi wanafanya kama kakitu cha mchezomchezo tu.

1. Ongeza mtaji wako mkuu, station nyingi za pesa za mtandao zina shida ya pesa, ukienda kuweka ama kuchua hata laki tano unaweza kuzunguka mpaka uchoke na solution iliyopo ni kuweka au kuchukua nusunusu, hivyo jaribu kuwa na mtaji mkubwa kiasi kwamba watu watakuwa wanakuja kwako wakijua hawatakwama

2. Ongeza Muda wa kazi, ufungue mapema sana na kufunga late ili hicho kijiwe chako kiwe kimbilio la watu wengi,

3. tafuta wafanyakazi wenye uzoefu na wenye lugha ya kibiashara

Hiyo biashara nzuri sana
 
Mtaji wako kwanza ni shilingi ngapi?Tusije tukaanza kutiririka kumbe hata kwenye hiyo tigo pesa na Mpesa mtu akija kutoa laki moja unasema hela kwenye account hamna

Million 1.3
 

Ahsante Sana Mkuu, Nimelipenda Wazo Lako Nitalifanya Kazi.
 
Jaribu kuuza pombe ili wakija kudraw waanze kutumia hapohapo!
 
Kwanza ni lazima uhakikishe kwamba Biashara mpya haififizi ile ya awali.
Unaweza kukuta unaunganisha Biashara halafu ikaififiza ile ya mwanzo nawateja kutokujua kwamba unafanya nini.Tegema wateja wapya na sio uwe na concept kwamba watu wanakujua unafanya nini.
Pia muda ambao ueanza hizo huduma ni miezi mitatu ni michache sana ku study Biashara.
Ila unaweza kufungua biashara ya Matunda(Fruits)mbali mbali na Juices,soda,Maji na Snacks nyingine.
 

Hili wazo ni zuri sana .
Ila mie naona tatizo la mtaji mkubwa wa kazi hizi ni usalama wa eneo husika.
Maana mtu akiwa na 1 au 2m tu roho juu.
 
Jaribu kuuza pombe ili wakija kudraw waanze kutumia hapohapo!

Mkuu Jirani Hapo Nilipo Fremu Ni Ya Kati Kati Kushoto Anauza Bia, Soda Na Ya Kulia Kwangu Naye Ivyoivyo.
 
Hili wazo ni zuri sana .
Ila mie naona tatizo la mtaji mkubwa wa kazi hizi ni usalama wa eneo husika.
Maana mtu akiwa na 1 au 2m tu roho juu.

ni kweli lakini, inabidi gharama za kuirekebisha ofisi kuwa kwenye mazingira ya usalama ni muhimu sana, kwa sababu jamaa anasema ana chumba kikubwa kinachotakiwa kufanyika ni kuigawa ofisi katika sehemu mbili, kunakuwa na chumba cha wahudumu ambacho kinakuwa kimefungwa muda mrefu na huko ndio kunakuwa na cash na document zingine na sehemu iliyobaki anaweza kuweka kakochi la kukaa hata watu watatu wanaosubiri huduma,

Mara nyingi kuvamiwa na kuibiwa sehemu kama hizo ni lazima kuwe na collution kati ya hao wezi na mtu wa karibu kabisa na hiyo biashara, wanaovamia hawaji kubahatisha wanakuja na full information kuwa kuna Hela kiasi fulani ndani

hivyo muhudumu wako lazima awe trustfull na labda lazima uchukue detailz zake kwa umakini, hiyo ni ajira so lazima ujiridhishe na mfanyakazi wako

Pili ni kuzuia hilo eneo kuwa kijiwe, mara nyingi vijiwe vingi vya Mpesa vinakawa ni kama Saloon, unakuta watu wamekaa na kupiga soga tu asubuhi mpaka jioni huku wengine wasoma movement ya cash na ndio hao huwa wanapanga mipango ya kukuibia

Siri ya biashara nayo ni muhimu sana, unaweza ukawa unaamisha cash kwenda bank na hakuna mtu anayeweza kujua, na pia Hasara au faida yako inakuwa ni siri ya ofisi na sio habari ya kila mtu
 

Wazo Zuri Mkuu, Kuhusu Uzoefu Wa Hii Kazi Ninao Wakutosha Koz Nilifanya Kwa Mtu Mda Mrefu Kidogo Kabla Ya Kuamua Kufungua Ya Kwangu, Ila Ahsante Kwa Ushauri Wako.
 
Hili wazo ni zuri sana .
Ila mie naona tatizo la mtaji mkubwa wa kazi hizi ni usalama wa eneo husika.
Maana mtu akiwa na 1 au 2m tu roho juu.

Kweli Mkuu, Maana Watu Wakishakuja Mara 1,2 Akaweka/kutoa Mil 1, 2, basi watajua yule jamaa ana mpunga mrefu.
 
kabla ya ushauri wa kitaalamu kwanza jibu maswali haya
mtaji wako ni sh ngapi hata kama huna sema ule uwezo wako wa mwisho ni ngapi
wananchi wako wana hali gani kiuchumi na kielimu kwa ujumla
Idadi ya wakazi wa mtaa wako ni kawaida au wengi kiasi au crowd of people
 

Nina Mtaji Wa Milion 1.3, Eneo Ambalo Nipo Lina Wakazi Wengi, Kuhusu Uwezo Wa Wananchi Kiuchumi, Wengi Ni Wananchi Wa Kipatao Cha Kawaida, Na Lina Wafanyabiashara Wengi Ambao Wanafanyabiasha Zilizoeleka Kama Maduka Ya Jumla, Rejareja, Ya Vinywaji, Magenge Na Uwakala Pia, Ndomaana Nilikuwa Nahitaji Wazo Tofauti La Biashara Ambalo Litakuwa Tofauti Na Biashara Zinazofanyika Hapa.
 

Na kwakuongezea ipo chance ya kupata kamkopo atleast ata wa lak 5 kama itanibidi.
 
Kuna kitabu kinaitwa 'Ujasiriamali kwa vitendo' linauzwa Tsh 5,000/- sabasaba. Kina biashara Kama 300 yameelezwa kwenye kitabu.
 

Mkuu hii biashara unafaham vizuri kuliko mleta uzi!! Mleta uzi anaijua hii biashara kwanjenje tu' na hajawahi fanya biashara nyingine..

Mkuu mleta uzi fata ushauri wa mdau hapo juu!! Mim pia nina kibiashara kama hicho na bahati nzuri kipo maeneo ya karibu na hapo ulipo!! Nachokiona kwako ni kwamba mtaji wako haujitosherezi' pia kama upo maeneo ya pale kwamsuguli pembezoni mwa barabara ya morogoro usijiroge ukachanganya na biashara nyingine' hapo utapoteza wateja wengi zaidi. Boresha biashara hiyohiyo, pendezesha ofisi yako na huduma nzuri na za uhakika kwawateja! Ukifanya hivyo hautojuta kamwe.!

Alafu nilikua natafuta frem eneo hilo' vipi uwezekano wa kupata upo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…