Kiungo wa Yanga MO BANKA afungiwa na CAF kwa kuvuta bangi

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
Kamati ya kuzuia na kupambana na dawa zisizoruhusiwa michezoni ya Kanda ya Tano Afrika (RADO) imetoa hukumu ya kumfungia mchezaji Mohamed Issa banka kutokana na matumizi ya dawa zisizoruhusiwa michezoni aina ya Bangi.

Kutokana na hilo Banka alitakiwa kutoa maelezo ikiwemo kukataa au kukubali kosa ambapo alikubali mashtaka hayo kwa kukiri kosa akichagua kujitetea kwa njia ya maandishi, utetezi aliouwasilisha Agosti mosi mwaka huu.

Baada ya uchunguzi wa maabara na utetezi toka kwa mchezaji huyo, Kamati imemkuta na hatia na imemfungua kwa kipindi cha miezi 14 kuanzia Disemba 9, 2017 na adhabu inatarajiwa kumalizika Februari 8, 2019.

Msemaji wa TFF Clifford Ndimbp ameeleza kuwa wakati wote Banka akitumikia adhabu hiyo hataruhusiwa kufanya chochote kinachohusiana na mpira wa Miguu, ikiwemo kufanya mazoezi hadharani au kuonekana akishiriki shughuli za mpira wa miguu.

TFF imesema kuwa mchezaji huyo alitakiwa kukutana na adhabu kubwa zaidi ikiwemo kufungiwa maisha lakini kamati kwa mamlaka iliyonayo imepunguza adhabu hiyo kufikia miezi 14 baada ya kumuona Mohamed Issa ni kijana mdogo.

Kwa upande wake Mohamed Issa amekiri na kujutia kitendo alichokifanya cha kutumia Bangi na ameahidi kuwa balozi mzuri kwa wengine wanaotumia dawa hizo zisizoruhusiwa michezoni.

Mnamo Disemba 9, 2017 Mchezaji huyo akiwa Machakos nchini Kenya alichukuliwa vipimo vya mkojo ambavyo vilisafirishwa kwenda kwenye Maabara ya WADA iliyopo Doha, Qatar kwa uchunguzi zaidi na majibu kurudi yakiwa na tuhuma hizo zinazomkabili.
 
Huo mdomo unaonesha tu.
Yondani nae anapimwa lini?
wasimsahau Mkude ,Said Nduda na Haruna Bobani
 
Michezo inahitaji nidhamu ya hali ya juu sana pamoja na kujituma ili ufike mbali.
 
Challenge si bonanza tu...inakuwaje adhabu kubwa hivyo
 
Shenzi mmoja, kama kawaida yetu starehe mbele kuliko kazi.
 
Hii ndumu kwa wachezaji wa bongo ni shida.
 
Huo mdomo unaonesha tu.
Yondani nae anapimwa lini?
wasimsahau Mkude ,Said Nduda na Haruna Bobani
Acha kumsingizia kiungo bora kabisa east Africa Jonas Gerald Mkude wavuta bangi wapo Yanga tu
 
Reactions: Tui
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…