Kiungo wangu bora wa ' Ukabaji ' nchini Tanzania kwa sasa Jonas Gerald Mkude a.k.a Deco De Souza amuumbua ' Mpuuzi ' Amunike

Hata mechi na UD SONGO yeye ndie alifanya turn akapoteza mpira then akacheza rafu

Hivi kuna Kiungo bora na mahiri yoyote yule duniani asiyecheza Rafu? Halafu leo ukimtuhumu Mkude kuwa ndiye katufungisha dhidi na hao Wamakonde wako mbona Siku ile alipofunga lile Goli lake la ' Muwa / Shuti / Bomba ' dhidi ya Nkana Uwanja wa Mkapa na kuisaidia Kuivusha Simba SC katika Klabu Bingwa sikukuona ukija hapa Kumpongeza? Mnafiki mkubwa Wewe! Na usivyojua Mpira yaani hadi leo hujui na hujajua kuwa Mpira ni Mchezo wa Makosa na ndiyo maana unashangaa kwa Mkude kufanya hilo Kosa. Hebu wapishe Watu wanaojua Mpira ninabadilishane nao Uzoefu hapa na Wewe usiyejua Mpira kaa Kimya ili angalau uweze Kujifunza mawili matatu kwani kwa hii ' Comment ' yako tu hapa umeshaonyesha kuwa hujui Mpira na si ajabu hata Uwanjani kwenyewe huwa huendi vile vile.
 
Mkuu huu ni mpira tu naona umehamia kwenye matusi, sijabisha kuwa mkude ni kiungo mzuri lakini kuniambia ndio kiungo bora mkabaji kwa hapa Tz ndipo nnapobisha, usitake kufanya maneno ya Aden Rage kuhusu mashabiki wa simba yaonekane ni kweli niishie hapa, nashukuru kwakunitusi
 
Mkude anamapungufu yake mara nyingi amekuwa off kwenye eneo lake angalia goli waliofunga Burundi yeye alikuwa wapi ,tuangalie mchezaji mmojammoja
Hawa vilaza wanaangalia zile back pass tu,awaangali wale burundi walivyokua wanacheza kimipango mpaka kutufanya sisi kama ndio tupo ugenini
 

' Takolingi ' ndiyo Lugha gani? Kimekushinda nini kuandika tu ' Tackling ' Ndugu? Halafu naomba kujua ulijifunza wapi au nani alikudanganya kuwa Kiungo yoyote Mkabaji ni lazima awe anafanya hizo ' Takolingi ' zako? Hivi Ngolo Kante huwa anafanya hizo Takolingi? Marehemu na Kipenzi changu kabisa kutoka nchini Cameroon Marc Vivien Foe alikiuwa akifanya hizo Takolingi zako? Kiungo mwingine wa Ukabaji Rafiki yangu ( sasa Marehemu ) Patrick Tabu Mutesa Petit Mafisango ( Baba Crespo ) Yeye alikuwa akifanya hizi Takolingi zako? Akili zako za ' Kipa Katoka ' hazipishani na alizokuwa nazo Kocha wenu ' Mpuuzi ' na niliyekuwa namchukia kuliko maelezo Emanuel Amunike.
 
😀😀😁 Umepanika mjomba Lete takwimu za mkude hasa za takolingi ,pia wewe amunike humjui

Ni kweli kwa Uwezo wangu wa Kimpira ambao naujua vile vile siwezi Kumjua ' Mpuuzi ' aitwae Emanuel Amunike na nilimchukia mno.
 
Kiungo bora wa baadae ni Ally nganzi

Endapo tu atakuwa Mjanja na upesi atakuja Kuichezea Simba SC ambayo ndiyo imebarikiwa na Mwenyezi Mungu kwa Kuwaibua na Kuwatengeneza Viungo bora kabisa hapa nchini Tanzania ambao mifano yao ipo mingi tu na wala sina haja ya Kuwataja hapa. Tangia lini Yanga SC ikawa na Historia ya kuwa na Viungo mahiri na bora. Walibahatika tu kwa Kaka yangu Athumani Abdallah China na Issa Athumani Mgaya ila tangia hapo hawajatoa Viungo wengine wazuri. Yanga SC ina bahati mno ya Kutoa Washambuliaji wazuri pamoja na Mawinga mahiri na Kidogo Mabeki ila kwa Simba SC ni Viungo na Makipa.
 
Kiungo bora wa Tanzania ni Fei Toto

Naziomba haraka sana zile Mamlaka ambazo zinahusika na Uzuiaji wa Ulimaji, Uuzaji na Matumizi ya Bangi nchini Tanzania ziongeze Juhudi kwani Bangi bado zinaendelea Kuathiri Akili za Watanzania wengi na mfano bora ukiwa ni huyu Laki Si Pesa hapa.
 
Kwahiyo angekwepo mkude kule Misri tusingefungwa?

Huenda angeyapunguza Magoli na hata Kusababisha Washambuliaji wetu nao Wafunge Magoli hasa kutokana na Uwezo wake wa Kujua Kuwachezesha na Kuichezesha Timu. Mtu yoyote ambaye anaujua vyema Mpira na pia amebahatika Kuucheza vile vile hatonishangaa An Eagle kwanini namsifia na namkubali kuliko Maelezo ' Mwanangu ' mwenyewe Jonas Gerald Mkude a.k.a Deco De Souza.
 
Shaaban nditi anamzidi mbali sana jonas mkude,
Nditi ana utulivu sana wa akili na mwili.
Nditi tangia akicheza mpira wa makaratasi hajawai kukosea kwenye nafasi ya kiungo,
Nditi 95% = Mkude 75
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Shaban Nditi ajifunze kwa mkude? Labda kama mimi siujui mpira

Ukiambiwa uwataje Viungo bora wa Ukabaji nchini Tanzania utamtaja huyu Shabaan Nditi wako? Hivi huoni hata Aibu tu unavyokjichoresha hivi kwa tunaojua Mpira vyema? Mimi ninachojua tu ni kwamba Shabaan Nditi ni Mchezaji Mkongwe, asiyejielewa, aliyechelewa na anayelazimisha Kucheza Mpira wakati Mpira haumtaki tena.
 
Sasa mtu kazaliwa 1990-1995 unataka awe ameanza kufuatilia lini mpira kama si 2000+. Hata ww wa miaka ya 70+ ulianza kufuatulia miaka ya 80+. Na si kigezo cha kuelewa zaidi
 

Nitajie Tusi katika hiyo ' Comment ' yangu tafadhali. Nasubiri nilione hilo Tusi unalosema kuwa nimekutukana nalo Ndugu sawa?
 
Shaaban nditi anamzidi mbali sana jonas mkude,
Nditi ana utulivu sana wa akili na mwili.
Nditi tangia akicheza mpira wa makaratasi hajawai kukosea kwenye nafasi ya kiungo,
Nditi 95% = Mkude 75

Akili yako ya ' Kipa Katoka ' ni kama aliyokuwa nayo Mwenzako ' Mpuuzi ' Kocha niliyekuwa namchukia mno Emanuel Amunike.
 
huna akili wewe nkajua unajielewa kumbe ovyo kabisa

Hata kaseja Juma mlikuwa mnasema hivohivo Nenda kabishane na wajinga wenzio, over
 
Nitajie Tusi katika hiyo ' Comment ' yangu tafadhali. Nasubiri nilione hilo Tusi unalosema kuwa nimekutukana nalo Ndugu sawa?
Kama hujaona tusi kwenye comment yako we mpumbavu siwezi bishana na mpumbavu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…