Kiungulia

Magnificient

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2013
Posts
1,162
Reaction score
705

Tumboni kwetu kuna kemikali kali ambayo ina uwezo wa kuunguza ngozi, msumali, sakafu, karatasi na kadhalika kama ambavyo unaona mtu akiwa amemwagiwa maji ya betri (Asidi ya salfyuriki). Kemikali hii ni asidi, na hujulikana kama asidi ya haidrokloriki (Kwa kiingereza huitwa Hydrochloric Acid). Sasa asidi hii huwa kama maji, na pia kwa juu huwa na mvuke kama unavyoona maji ya moto yakichemka na mvuke juu. Asidi hii ni muhimu sana kwa maisha yetu kwa sababu inasaidia katika mmeng'enyo wa chakula, inasaidia kuua vijidudu vya magonywa vilivyofika tumboni na chakula na kadhalika. Asidi ya majimaji hukaa tumboni, ila huo mvuke ndo huweza kupanda juu ya tumbo hadi kwenye koo na kumfanya mtu ajisikie kama anaungua - Hicho ndicho kiungulia sasa! Yaani kiungulia ni ile hali ya kuhisi kuungua kooni kunakosababishwa na mvuke wa hiyo asidi.Hicho ndicho kiungulia rafiki......

USHAURI
Ukipatwa na kiungulia unaweza kukituliza kwa kutumia dawa au kitu kitakachopambana na asidi na kuweza kuipunguza ukali na kuondoa mvuke wake.
Moja kati ya dawa hizo ni Vidonge vya Magnesium au Magnesium ya maji.
Pia kama kwa dharura na hizo dawa huwezi kupata basi jivu huweza kusaidia.
Changamoto kwa jivu ni kwamba linaweza kuwa chafu na vijidudu vya magonjwa.
Pia huwezi jua limetokana na mti gani, baadhi ya miti ina sumu,
Kwa hiyo sikushauri sana kutumia jivu kwa ajili ya kiungulia, ila nakushauri uwe na akiba ya Vidonge vya Magnesium.

Pia kama unasumbuliwa na kiungulia basi epuka vyakula vinavyochochea kuzalishwa kwa kiasi kikubwa cha asidi ambayo hatimaye itapelekea mvuka utakaopanda na kukuunguza kooni
Mifano vya vyakula hivyo ni maharage, kande, vyakula vilivyolala, mkate, kahawa na kadhalika
Ukifanya hivyo maisha yako yatakuwa mazuri na kiungulia hakitakusumbua

NB:
Nimecopy na kupaste kutoka AFYA ZAIDI Consultants (Ukurasa wa Facebook)!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…