kiungulia

Nkabahati

Member
Joined
Feb 6, 2012
Posts
12
Reaction score
2
Habari wanajamii. Mimi huwa nasumbuliwa sana na kiungulia, nikiwa mjamzito huwa kinazidi. Nini husababisha kiungulia? na ninini dawa ya kiungulia? Naomba mnielimishe!
 
Natamani kufahamu pia, kiungulia kinanyima raha kabisa.
 
Husababishwa na kujaa gesi(tindikali) tumboni,ujauzito hupunguza nafasi ya tumbo na kufanya umeng'enywaji wa chakula kutokuwa vizuri na hivyo tindikali (hcl) kuzidi! Tumia Relcer gel au Magnesium yoyote ya maji kama nimekosea nisahihishwe
 
Unaweza kutumia Omeprazole au Lansoprazole, zitakusaidia.
 
Ni acidity nadhani... jaribu kunywa maziwa ya mgando (yogourt)
 
Punguza kula ndimu maembe maharage,acid imezidi tumboni,kunywa maziwa kunyutrolaizi
 
Maziwa fresh ni bora zaidi. Yanapofika tumboni yananeutralize acid na kuganda.
>kunywa maziwa mara kwa mara kama kinga,usisubiri hadi kiungulia kije.

> epuka vitu vichachu na vyenye acid,km vidonge vya asprin,limao,ndimu

> epuka kushinda na njaa muda mrefu.
 
wakuu me nakunywa maziwa glasi moja paka mbili daily,cinywi soda sana,nakunywa juice ya maembe,passion,nunus nk: lakini napata hiyo kitu sana,tatizo nini? Hakuna tiba permanent?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…