Salaam alaikum,
Kijana wa chuo,kijana wa kiume ambaye familia yake ilitegemea apate elimu Kisha kupitia elimu hiyo ukombozi wa kiuchumi upatikane kwa wanaomtegemea,ameamua ajirushe gorofani kisa chipsi alizomnunulia mpenzi wake.
Iko hivi, jamaa ana mpenzi wake chuoni na kwa alivyokuwa anaona yeye nikwamba alikuwa anapendwa,ama tuseme walikuwa wanapendana. Siku ya tukio mdada yupo chumbani(wote wanaishi hostel),akampigia jamaa kwamba anaumwa na chakula anachojisikia kula ni chipsi kuku na Azam embe ya baridi.
Kijana katika Hali ya kujali akavinunua hivyo vitu akapeleka chumbani kwa mdada na kumkabidhi huku akimsisitiza mpenzi wake ale ili arejee kwenye Hali yake ya kawaida. Mdada akadai hajisikii kula kwa muda ule hivyo jamaa amuache tu atakula badae kidogo. Baada ya stori mbili tatu kijana akaondoka kwa kuwa tayari ilikuwa ni usiku.
Aiyaaa! kufika katikati ya safari akagundua kasahau ufunguo wake pale alipokuwa hivyo ikabidi arudi. Wakati yupo nje ya chumba akasikia mdada anacheka na anaaongea kwa bashasha kama vile sio yeye aliyekuwa mgonjwa. Kijana akiwa anaamini kuwa chipsi zimeleta uponyaji wa gafla kwa mpenzi wake akaamua kuingia bila hata kugonga mlango ili aungane na mwenzake kwenye hiyo furaha then achukue funguo zake aondoke.
Kuingia anakutana na njemba imekalia zile chipsi huku wakilishana na yule mdada kwa raha zao. Kilichofuata jamaa aliyeleta chipsi alitoka akaaenda gorofa ya 3 ya jengo lile akajitupa chini. Uzuri hakufa ila kiuno na mgongo havileti matumaini kwamba Kuna siku atatembea tena. Yupo hospitali na kwa kiasi kikubwa wazazi wake ndo wanabeba garama za matibabu kwani Ile bima imeshindwa kugharamia kila kitu.
Tuwaambieje hawa vijana kuhusu mapenzi?