Kiuno na mgongo

Makambuya

Member
Joined
Dec 6, 2011
Posts
45
Reaction score
3
Jamani wana JF wenzangu naombeni msaada mwenzenu kiuno na mgongo vinaniuma sana hasa nikiwa nimelala au kukaa kwenye kiti.
 
Tatizo lenu vijana wa siku hz mnapenda sana ...,* jaribu kufanya mazoezi, maumivu ya kizidi muone dk kwa ushauri zaidi.
 
Una umri gani? Na ulishawahi kupata tatizo kama ajali vile?
Pole ngoja tusubiri madoctor maana mgomo umekwisha
 
Mazoezi muhimu sana dalili za overweight.

Pili kuna viti vingine ukikalia vinaumiza kiuno na mgongo pia magodoro mengine yanaumiza mgongo,jaribu kuangalia hilo swala.
 
Una umri gani? Na ulishawahi kupata tatizo kama ajali vile?
Pole ngoja tusubiri madoctor maana mgomo umekwisha

asante ndugu yangu, mimi nina umri wa miaka 25 na sijawahi kupata tatizo lolote la ajali.
 
Mazoezi muhimu sana dalili za overweight.

Pili kuna viti vingine ukikalia vinaumiza kiuno na mgongo pia magodoro mengine yanaumiza mgongo,jaribu kuangalia hilo swala.

Kaka mazoezi nafanya labda kuwe na mazoezi maalu. mh! suala magodoro, hilo nalo neno. nashukuru sana.
 
[h=2]Dawa Ya Wenye Kuumwa Na Mgongo[/h]


Gundi ( hili gundi limekaa kama ubani wa kufukiziya ) ukiwaambia wenye kuuza madawa wanafahamu. Unasaga unakuwa unga.
Lozi ( unaroweka kwa maji ya mfukuto kisha unatoa maganda na unazikausha kidogo kwenye oven kisha unazisaga.)
Sukari ya Mawe au sukari guru (sukari nyekundu)
Hiliki
Za'fani
siagi kidogo
Maziwa

** Unayayusha siagi yako kisha unatia sukari (mawe au guru) kisha unatia lozi unachanganya kisha unatia gundi, hiliki na za'faran. unaiyepua unaitia kwenye sinia.

*** Ikisha kupoa unatia kwenye chupa au pahala kuihifadhi.

NAMNA YA KUTUMIA:- Kijiko cha supu kimoja asubuhi utakula na usiku kimoja.
MAZIWA UTAKUNYWA GILASI MOJA ASUBUHI BAADA YA KWISHA KULA HIYO DAWA NA USIKU GILASI MOJA BAADA YA KWISHA KULA DAWA.​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…