Kiutani zaidi msimaindi! Watani zangu wana Kagera eti ni kweli kwamba..

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Sababu kuu ya kutokewa na lililowatokeeni majuzi huko kwenu Kagera ni baada ya " vurugu " zenu kubwa zinazojulikana tokea enzi na enzi mlizozifanya usiku kucha wakati wa Tamasha la Fiesta eneo maarufu la " katerero " hivyo Mababu na Mabibi zenu " walikasirika " na kuamua kuwaadhibu kama walivyowaadhibu?

Sasa mnataka tuwachangieni ila nadhani mnatambua kabisa kuwa huku kwetu Mkoani Mara zao letu kuu ni Cannabis Sativa a.k.a Urithi wa Bob Marley je mnataka tuwaleteeni huko Kipindi hiki ili " mlanduke " zaidi ili iwe kama " ganzi " kwenu na mpate usingizi kwani tunaambiwa kwa sasa hampati kabisa usingizi.

Wana Mkoa wa Mara sasa tunajipanga kuja kuwachukuwa Wanawake wa Kihaya ambao mara nyingi sana huwa " wanaturingia " sisi wana Mara ila najua kwa shida na njaa za sasa " tutawabeba " wengi mno na kuja kuwahifadhi, kuwaoa na kuwazalisha huku kwetu Mkoani Mara.

Watani zangu wa Mkoani Kagera Wahaya bhana....hivi kwanini Mkoa wa Mara hatukumbwi na " majanga majanga " kama haya yanayowatokeeni nyie mara kwa mara?

Njooni " mtubu " dhambi zenu kwenye Kaburi la Mtani wenu Mkuu Baba wa Taifa huku Butiama ili awaombee " msamaha " kwa Mwenyezi Mungu na msitokewe tena na " mabalaa " kama hayo. Nasikia mnalalamika hamna chakula hivi wale " senene " sasa hawaruki ruki tena hapo katika Viwanja vya Kashai? Safari mtakula hadi " panzi " kudadadeki zenu.

Kama Wewe ni Mwana Mkoa wa Mara tafadhali karibu uendeleze " utani " wetu dhidi ya hawa Wajomba na Shangazi zetu wana Mkoa wa Kagera. Wakora waitu wote!
 
Sawa mtani..... Ila hilo zao la huko kwenu ni la local sana sisi tumezoea ile kitu manjuana ya kimataifa
 
Wewe limekukosa kweli? Bahati yako! Halafu mbona Wahaya mliopo hapa Dar hamtualiki sisi Wana Mara tuje kuwafarijini? au mnatuogopa kwakuwa tunakula sana Ugali mkubwa na Nyama nyingi hivyo Ukata huu umewatieni umasikini?
 
Hivi kumbe utani wa kikabila unaweza kufika hadi kwenye issue tata kama hizi?
 
Sisi hatuwezi kuwa maskini kwa suala dogo kama hili....
 
Hivi kumbe utani wa kikabila unaweza kufika hadi kwenye issue tata kama hizi?

Tena hapo nimewasamehe tu Wana Kagera. Tafuta au jaribu hata siku moja tu kuhudhuria msiba wa Mhaya na Kabila lolote lile lililopo Mkoani Mara ( Musoma ) utakumbana na makubwa tena zaidi ya haya. Nakumbuka miaka ya 95 hadi 97 hapo Familia ya Baba wa Taifa kule Butiama ilipatwa na Msiba nadhani na Ndugu tu wa Ukoo sasa ungekuwepo pale nadhani badala ya kulia ungeishia tu kucheka kwani kama kawaida yao Watani zetu Wahaya walijazana na nakumbuka walikuwa wakimpiga " madongo " mubashara Mwalimu na Wazanaki wote tuliokuwepo pale kuwa sisi ndiyo tumemuua Marehemu ili tutambike vizuri Ng'ombe zetu zisiibiwe na nakumbuka kuna Mzanaki mmoja sijui ni katika kukosea au kutokujua kuwa tuna utani na Wahaya akawatukana tusi la Nguoni kabisa tena la kudhamiria. Wakati wengine tulikuwa hatujui hili na lile ukafika muda sasa wa kubeba mwili kwenda kuuzika yule yule Mhaya aliyetukanwa akawahi lilipokuwepo Jeneza na kulikalia juu kitako kabisa kisha mbele ya Walinzi wa Mwalimu akina Mzee Mkanzabi na wenzake akasema kuwa ule mwili hauwezi ukaondolewa pale ndani hadi Wazanaki tulipe faini ya yeye kutukanwa. Mkuu huwezi amini Wazanaki wote pale tulianza kuchangishana Hela na ilipotimia ile Hela aliyoitaja tukamkabidhi yule Mhaya lakini cha ajabu akaikataa ile Hela na kusema ni ndogo na aongezewe ndipo Mwalimu baada ya kuona maji yametufika Shingoni Wazanaki akaamuru Watu wakimbie zizini wakatafute Ng'ombe aliyenona waje nae pale eneo tulilokuwepo kisha akabidhiwe kwa yule Mtani wa Kihaya ndipo kweli alipoletwa yule Ng'ombe Mtani wetu akashuka juu ya lile Jeneza na kuturuhusu kuubeba mwili kwenda kuuzika. Hata hivyo unaweza kuona Utani ni upuuzi ila nakuambia katika misiba au sherehe mbalimbali hakuna Watu wanaojitolea kufanya Kazi kama Watani na binafsi naupenda mno utani huu wa Kikabila.
 
Mimi sio mtani wa wahaya Ila najiuliza tu ule usikuu wa tetemeko ilikuwaje kwa wale waliokuwa wana practice KAGTECH?
 
MUNGU WANGU!...Mkuu kumbe mambo ndo yapo hivi?...nimebaki bila maneno baada ya kusoma ushuda wako.

Sawa MKuu kila la kheri kwenye huo utani wenu.
 
Back
Top Bottom