A
Anonymous
Guest
Ukifika kivuko Cha Busisi mkoani Mwanza unakuta tangazo kuwa kuna changamoto ya chenji ya Sh mia, ukichungulia mezani kuna silver za mia Tano na mia mbili, nauli ya kuvuka ni TSH 400 kwa mtu mzima lakini ukitoka sh 500 unapewa risiti yenye thamani ya 400 inayobaki hupewi.
Je, huwa wanazipeleka wapi hela zinazozidi?, ukiangalia wanaovuka kwa siku ni wengi sana na sio wote wanakuja na sh. 400 kamili, kama kuna changamoto ya chenji kwanini wasitengeneze tu risiti za TSH 500 kuliko hizo sh 100 zinazobaki na hazina maelezo zimepatikana vipi maana pesa yenye maelezo ni ile iliyokatiwa risiti
Naishauri serikali kufatilia hili jambo ili wananchi wasizid kupoteza chenji zao.