Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
TAFSIRI YA KISWAHILI ''KUVULI CHA BABA ZAO KINAPOWAFUNIKA WATOTO NA WAJUKUU''
Serikali ya kikoloni ilikuwa kila kukicha inabadili mitindo, hila na mbinu za ukandamizaji ili kuendeleza utawala wake.
Ukitazama mwelekeo wa siasa na mazingira ya wakati ule, uongozi wa wazee katika TAA, kwa hali yao na kutokana na mambo yaliyokuwa yakiwakabili, walikuwa hawana uwezo wa kukabiliana na changamoto ya ukoloni.
Lakini pamoja na yote hayo, wazee hawakutaka kuachilia madaraka.
Jambo hili lilizusha mvutano baina ya wazee na wanasiasa vijana waliosomeshwa na himaya ya Waingereza.
Vijana hawa walikuwa akina Abdulwahid na Ally Sykes, Tewa Said Tewa, Stephen Mhando, Dossa Aziz, James Mkande, na wale madaktari watano - Joseph Mutahangarwa, Luciano Tsere, Michael Lugazia, Vedasto Kyaruzi na wengineo.
Haya yalikuwa ni mapambano baina ya kizazi kipya na kile cha kale.
Katika mvutano huu wa madaraka kwa upande wa vijana waliokuwa wakiinukia alikuwepo kijana wa Kidigo kutoka Tanga aliyesomea Makerere, Hamza Kibwana Mwapachu.
Mwapachu alikuwa ameajiriwa na Idara ya Maendeleo ya Jamii kama 'Assistant Welfare' Officer (Msaidizi wa Ustawi wa Jamii), Ilala Welfare Centre mjini Dar es Salaam.
Historia ya Mwapachu katika siasa inaanza Makerere College, Uganda ambako alijihusisha na mambo ya siasa wakati alipokuwa mwanafunzi.
Mwaka wa1947 Mwapachu akiwa Tabora alichaguliwa kuwa katibu wa African Association, Julius Nyerere akiwa naibu wake.
Huu ulikuwa ndiyo wakati Wasomi wa Makerere walikuwa wameanza kujishughulisha na chama.
Mwapachu na Abdulwahid walikuwa na usuhuba mkubwa.
Mwaka wa1950 Mwapachu alikuwa na umri wa miaka thelathini na mbili na Abdulwahid alikuwa na umri wa miaka ishirini na sita, mdogo kwa Mwapachu kwa miaka sita.
Vijana hawa wawili walikuja kugeuza mwelekeo wa TAA na wakaingiza ndani ya chama hicho aina mpya ya uongozi uliokuwa haujapata kuonekana katika historia ya Tanganyika.
Lakini wote wawili walifariki dunia katika ujana na wote wawili wakaja kusahauliwa na historia.
Hakuna kati yao ambaye hii leo jina lake linahusishwa na historia ya Tanganyika ingawa walikuwa karibu sana na Julius Nyerere.
Vijana wa Makerere walipokuwa wakifikiria jinsi ya kuleta mageuzi ya kisiasa nchini Tanganyika kupitia TAA, Abdulwahid alikuwa tayari amejijengea katika msingi wa siasa mjini Dar es Salaam.
Wasomi wa Makerere walikuwa wanakuja Dar es Salaam, baadhi yao kwa mara ya kwanza, kuanza kazi serikalini katika taaluma mbali mbali.
Wengi wao walikuwa Wakristo walioelimishwa na wamishionari.
Vijana hawa walikuwa na hadhari sana kuhusu siasa.
Walikuwa mbali na makwao na walikuwa ndiyo kwanza wanaanza maisha.
Walikuwa na matarajio ya kufaidika kutoka serikali ya kikoloni kutokana na nafasi zao kama watumishi wa serikali.
Juu ya hayo walitegemea vitu kama mkopo wa kununua magari na kupewa nyumba nzuri ya kuishi katika sehemu makhsusi Wazungu walizowatengea Waafrika kama hawa.
Nyumba hizi zilikuwa bora kuliko zile za matope na makuti za wanyeji wengi.
Kwa waliobahatika wangeweza kwenda Uingereza kwa mafunzo.
Waliamini kwamba kujishughulisha na siasa ilikuwa sawa na kuipinga serikali na jambo hili lingehatarisha kazi zao.
Wengi walihisi kuwa kuwa na mawazo ya kutaka kupambana na serikali ya kikoni ilikuwa ni jambo la hatari.
Hawa walikuwa vijana wasomi waliokuja Dar es Salaam kufanya kazi kisha wapate uhamisho wa kwenda sehemu nyingine.
Walikuwa wamesomeshwa ili wawe watiifu kwa serikali.
Hawa wasomi wa Makerere hawakutegemewa waje kuwa watu wasiokuwa na shukurani kiasi cha kuuma mkono uliokuwa ukiwalisha. Kwa watu kama hawa haikuwa rahisi kwao kuweza kuhisi ile dhuluma iliyokuwepo kutokana na ukoloni kiasi cha kutaka kuingia katika siasa na kuupiga vita utawala wa Waingereza nchiniTanganyika.
Abdulwahid alikuwa na kipaji cha kuongoza, alikuwa mtu wa kupendeka, mwenye tabia nzuri, mtu wa kuaminika na hakuwa mbinafsi.
Kwa muda mfupi Abdulwahid aliwachota wasomi wa Makerere kwa fikra zake, wakamwamini na taratibu akawatumbukiza ndani ya siasa za Dar es Salaam.
Abdulwahid alikuwa na uhusiano mzuri na Bohra Muslim Community wakati huo ikiwa chini ya uongozi wa Abdulkarim Karimjee ambaye alikuwa vilevile Meya wa Dar es Salaam.
Karimjee alikuwa akifahamiana na Abdulwahid kwa miaka mingi.
Tutaeleza huko mbele kwa undani mashaka yaliyokuja wasibu Waismailia na kiongozi wao Aga Khan baada ya uhuru kwa ajili ya Uislam.
Uhusiano wa Abdulwahid na jumuiya zote hizi na uongozi wake uliimarisha matumaini yake kuongoza na kuigeuza TAA kutoka chama cha siasa kilichojificha na kuwa chama cha siasa kilicho wazi katika malengo na madhumuni yake.
Abdulwahid alikuwa kijana mashuhuri na alijulikana takriban na kila mtu Dar es Salaam.
Ilikuwa kawaida akija mtu pale mjini kutoka bara alichukuliwa na wenyeji wake hadi nyumbani kwa Abdulwahid kwenda kujulishwa kwake na kwa njia hiyo ''kutolewa ukumbi.''
Hapo alipewa mwelekeo wa siasa na kukaribishwa katika harakati.
Huu ndiyo ule wakati vijana hawa walianzisha Wednesday Tea Club, kikundi cha vijana wasomi. Vijana hawa walikutana kila Jumatano jioni kujadili siasa huku wakinywa chai.
Nyumba ya Abdulwahid ilikuwa vilevile sehemu ya kukutania hawa vijana wasomi pamoja wa wake zao, kwa kula pamoja na kuburudika.
Halikadhalika Abdulwahid alikuwa na uhusiano mzuri na machifu wengi wa Tanganyika.
Machifu hao wakiwa Dar es Salaam kuhudhuria Baraza la Kutunga Sheria, Abdulwahid alichukua fursa hiyo kuwakaribisha nyumbani kwake kwa chakula cha mchana au usiku na wakati mwingine aliwafanyia dhifa.
Baadhi yao walikuwa Chifu Haruna Msabila Lugusha wa Sikonge, Mtanganyika wa kwanza kufuzu kama bwana shamba, Chifu Thomas Marealle wa Marangu, kwa sababu Abdulwahid alizoea kumtania kwa kumwita Marealle, ''King Tom.''
Waingereza walitaka Waafrika waamini kuwa ufalme ni wao pekee, Wazungu ndiyo walikuwa na mfalme, malkia, wana na mabinti wa mfalme.
Waafrika wangeweza kuwa na machifu tu.
Chifu David Kidaha Makwaia wa Shinyanga na wengine vilevile walikuwa wageni wa Abdulwahid nyumbani kwake.
Abdulwahid aliwakumbusha vijana wenzake kwamba hakuna kati yao aliykuwa na wadhifa wowote katika TAA, ambapo mijadala yote iliyokuwa ikifanyika nyumbani kwake juu ya Tanganyika ilipostahili kufanyika.
Abdulwahid, akikumbuka ahadi iliyowekwa mwaka 1945 kule Imphal nchini Burma ya kuunda chama cha siasa, mara nyingi sana alijadiliana na marafiki zake Mwapachu, Dossa Aziz na mdogo wake Ally kuhusu kutekeleza ile azma ya kuunda chama cha siasa ambacho kingewajumuisha watu wote wa Tanganyika.
Inasemekana Mwapachu na wengine wachache kama Stephen Mhando walikuwa na shauku sana na wazo hili lakini vijana wengi, hususan wale waliokuwa watumishi serikalini walikuwa na shaka iliyojaa hofu kuhusu wazo hilo.
Ofisi ya Mwapachu pale Ilala ikawa kituo cha mijadala ya siasa nyakati za mchana.
Jioni vikao hivyo vya majadiliano vilihamia Tanga Young Comrades Club.
Hii ilikuwa club maarufu ya kukutana, hasa kwa vijana maarufu na muhimu katika mji wa Dar es Salaam. Club hii ilikuwa New Street, Karibu na makao makuu ya TAA.
Mijadala ya siasa nyumbani kwa Abdulwahid au katika ofisi ya Mwapachu Ilala au Tanga Club kidogo kidogo ikawa inaingia katika nadharia ya vile vijana wangeweza kuitoa TAA kutoka kwa wazee wale, ambao kwa hakika vijana waliwaona kama makapi ya utawala wa Kijerumaini.
Wakati ule mwaka 1949, Mwalimu Thomas Plantan ndiye aliyekuwa rais wa TAA.
Katibu wake alikuwa Clemet Mohammed Mtamila.
Si kwamba Tanganyika wakati ule ilikuwa na uhaba wa maswala ambayo yangeweza kuamsha mijadala ya siasa.
Kulikuwa na mambo kadhaa ambayo kama yangetumiwa kwa ustadi na uongozi wa TAA, shida hizo zingeweza kuleta kwa watu hisia za manung'uniko na chuki dhidi ya serikali ya kikoloni.
Unahitaji tu kuzipitia tahariri za Mashado Plantan katika gazeti la Zuhra ili kuweza kufahamu mambo yalivyokuwa nchini Tanganyika katika miaka ya 1950.
Naye Mwalimu Thomas Plantan na damu yake ya Kizulu ya kupenda vita, baada ya kuwa yupo kwenye nchi yenye amani, aliielekeza banduki yake porini kuwinda wanyama.
Hakuwa na muda kama rais wa TAA kushughulika na siasa.
Uhodari wake katika kuwinda bado hadi leo unaweza kushuhudiwa nyumbani kwake Mtaa wa Masasi, Mission Quarters.
Kuta za nyumbani kwake zimeshamiri mafuvu ya vichwa vya wanyama aliowaua huko porini.
Kwa kuwa alitumia wakati wake mwingi porini akiwinda, hakuwa na muda wa kuitisha mikutano au kushughulikia mambo ya TAA.
Makao Makuu ya TAA mjini Dar es Salaam yalikuwa kama vile yamegubikwa na usingizi mzito.
Barua kutoka matawini hazikuwa zikijibiwa. Baya zaidi, hakukuwepo na mawasiliano yoyote na Baraza la Udhamini la Umoja wa
Mataifa mjini New York ambalo ndilo lilikuwa likiitawala Tanganyika kama nchi ya udhamini.
Hali ya wazee wa TAA ilikuwa na sura nyingi.
Schneider Plantan alikuwa amekwisha onyesha chuki yake dhidi ya Waingereza na kwa ajili hiyo akawekwa kizuizini wakati wa Vita Vya Pili.
Mashado Plantan alikuwa na gazeti lake Zuhra ambalo lilikuwa ndiyo sauti ya African Association.
Lakini watu hawa walikuwa wazee na wamechoka.
Hawakuwa na jipya katika siasa.
Walipochoshwa na uongozi huu wa wazee na walipoona hakuna lolote la maana liliokuwa siku moja wakati wa alasiri, Abdulwahid na Mwapachu bila ya kumshauri mtu yeyote wakitokea Tanga Club, New Street, na kuivamia ofisi ya TAA na kufanya mapinduzi kwa kumtoa msobe msobe Clement Mtamila ofisini kwake.
Abdulwahid alikuwa bingwa wa ngumi wa Tanganyika na Kenya katika kikosi chake wakati wa vita.
Hakupata tabu sana kumtoa nje ya ofisi Mtamila.
Baada ya vurugu wazee walisalimu amri na wakaamua kuitisha uchaguzi makao makuu ya TAA.
Mwezi Machi mwaka 1950, katika Ukumbi wa Arnatouglo, kijana wa Kihaya, Dr Vedasto Kyaruzi alichaguliwa kuwa rais na Abdulwahid Sykes katibu wake.
Walipochukua uongozi, TAA ilikuwa na shilingi 87.00 katika Barclays Bank.
Huu ndiyo ulikuwa mwisho wa wazee, kuongoza TAA.
Vilevile mwanzo wa uzalendo nchini Tanganyika.
Kuanzia siku ile, majina ya Abdulwahid kakake mdogo wake Ally na lile la Mwapachu yalianza kuhusishwa na makao makuu ya TAA na siasa zilizokuwa zikiibuka za uzalendo Tanganyika.
Abdul alikuwa sasa anajiondoa kutoka kivuli cha baba yake na kuwa mwanasiasa kutokana na mafanikio yake binafsi.
Abduliwahid alikuwa anaendeleza ile sifa ya baba yake ya kuwa mtumishi wa umma na jamii yake.
Taratibu aliaanza kujijengea himaya yake mwenyewe akisaidiana na 'wasomi wa Makerere.'
Baadhi ya wanasiasa wakongwe wengine washirika wa marehemu baba yake kama Schneider, Mashado Plantan na Clement Mtamila walimuunga mkono yeye na Kyaruzi katika kuipa TAA uhai mpya.
Kamati Ndogo ya Siasa Ndani ya TAA, 1951
Hakuna nyaraka zozote zinazoonyesha kama African Association ilikuwa imetayarisha mpango wa kushughulikia hali ya siasa.
Kuelewa mwelekeo wa siasa kama wakati ule inabidi mtu atazame mwenendo wa viongozi wa TAA na jinsi walivyokuwa wakiyashughulikia mambo tofauti yaliyokuwa yakiwadhili wananchi.
Jambo la kwanza alilofanya Abdulwahid mara tu baada ya kuingia madarakani ni kuunda TAA Political Subcommittee (Kamati Ndogo ya Siasa ya TAA) iliyomjumuisha yeye mwenyewe Abdulwahid, Sheikh Hassan bin Amir kama mufti wa Tanganyika; Dr. Vedasto Kyaruzi, Hamza Mwapachu, Said Chaurembo aliyekuwa liwali wa Mahakama ya Kariakoo; John Rupia na Stephen Mhando.
Kazi ya kamati hii ilikuwa ni kushughulika na masuala yote ya siasa katika Tanganyika.
Kuundwa kwake ndiyo hasa ulikuwa mwanzo wa siasa za dhahiri katika Tanganyika na mwanzo wa harakati za kudai uhuru wa Mtanganyika.
Picha: Kulia ni Abdul Sykes na Hamza Mwapachu.