Kiwanda cha Bodaboda

Mlenge

R I P
Joined
Oct 31, 2006
Posts
2,125
Reaction score
2,306
Kiwanda cha Bodaboda

Ikiwa kichwa cha habari kimekufanya uwaze mitambo ya kutengeneza pikipiki, karibu kwenye mada.

Mada hii si kuhusu mitambo ya kutengeza pikipiki (factory). Mada hii inahusu watoa huduma za usafiri wa bodaboda. Mafundi wa pikipiki za bodaboda. Watumia huduma za bodaboda. Na kiasi cha pesa kinachozunguka kila siku kutokana na bodaboda. Yaani, Kiwanda cha Bodaboda (Bodaboda Industry).

Fikiria iwapo leo hii serikali itapiga marufuku bodaboda. Kiwanda cha Bodaboda kitakwisha mara moja. Je, ni watu wangapi wataathirika kwa kukosa ajira na kukosa huduma? Je, tutaweza kumudu gharama za kukifunga kiwanda hicho? Bila shaka jibu ni hapana.

Mafanikio makubwa ya Tanzania ya Viwanda yameripotiwa kuhusiana na Viwanda ambavyo ni Factories. Hii imepelekea baadhi ya watu kudhani Viwanda ni vile tu vya mitambo. Pengine ni wakati muafaka wa kupembejea viwanda (industries) vya huduma kama sehemu ya mkakati wa Tanzania ya viwanda. Bodaboda ni mfano tu. Vibanda vya huduma ya pesa kwenye simu (M-Pesa/Tigopesa/Airtel-Money/Halopesa/T-Pesa...) nayo ni mfano wa kiwanda. Watu wangapi wameajiriwa na kiwanda hicho? Wangapi ni wanufaika? Ujazo wa mzunguko wa pesa ni kiasi gani? Serikali ikiamua kukifunga kiwanda hicho, wangapi wataathirika? Je, tutaweza kumudu gharama za kukifunga kiwanda hicho? Bila shaka jibu ni hapana.

Viwanda-huduma (service industries) zilizoko ziimarishwe, na nyingine mpya zihamasishwe kuanzishwa ili kuboresha utekelezaji wa sera ya viwanda, kama nyongeza ya mwelekeo wa kwenye viwanda-mitambo (factories).

 
Kiwanda cha Bodaboda ...
Safi sana, umefafanua vizuri. Tatizo langu ambalo kwa muda mrefu limekuwa linanitatiza ni jinsi gani Serikai inaweza kufanya hizi shughuli ziwe regulated vizuri zaidi. Mfano ajali za Boda boda ni nyingi sana na wengi wamepoteza maisha kutokana na waendeshaji kuwa hawana mafunzo (Yaani mtu anajifunzia humo humo baada ya mikasa kibao ndio anakuwa stadi).
Pamoja na mambo mengine kuna Watanzania ambao hawataki kabisa kusikia hizi boda boda kutokana na aidha ajali au kifo kwa ndugu na jamaa. How best can the Government come up with something to make this service better? Also to encourage other services which fit our situation.
 
Regulations stiffle industries. The less regulations, the more successful an industry becomes. Regulations are anachronistic to the current developments.

Madereva wa bodaboda waliofuzu vizuri, wanaojiona mahiri sana, ndio wako kwenye hatari zaidi kupata ajali kuliko wanaoanza, ambao huwa makini. Vijiwe vya bodaboda hujiwekea sheria zinazoboresha utendaji.

Eyes-on, Hands-off. Ndio approach ambayo itafanya industries zikue.

Kwenye upande wa Ardhi, serikali imefanya kazi kwa karibu na makampuni ya urasimishaji, na hivyo serikali kufikia maeneo mengi ndani ya muda mfupi. Modeli hii inaweza kurudiwa kwenye elimu. Makampuni yasajiliwe kutoa elimu ya msingi na sekondari kwenye majengo ya shule za serikali, na nje ya majengo hayo. Serikali ibakie kutunga sera. Mambo ya utekelezaji, iwaachie wananchi. Itaokoa gharama nyingi. Huduma bora zitatolewa.

Yaani, angalia mabenki. Siku hizi hukuti foleni ndefu benki kama zamani. Kwa vile mawakala wamejaa kila kona wakitoa huduma za msingi za kibenki. Na kwenye elimu ikifanyika hivyo, serikali itajikuta imeanzisha "Kiwanda cha Elimu" ambapo patakuwa na ushiriki mkubwa wa sekta binafsi kutoa elimu kwa niaba ya serikali. Sekta binafsi hujulikana kwa ufanisi mkubwa ikilinganishwa na sekta ya umma. Angalia Teacher-Pupil-Ratio za shule za umma na zile za binafsi.
 
Hili la regulations hapana. Tanzania tupo hapa kwenye huu umasikini kwa kutokuwa na regulations ambazo haziko wazi na nyingi ambazo hazifahamiki vizuri na watumiaji. Ajali nyingi zinatokea kwa sababu ya wengi kutokujua sheria zinasemaje. Nilikuwa Tanzania kwa mfano dreva niliyekuwa nae alipita kwenye Zebra crossing wakati watembea kwa miguu walikuwa wanataka kuvuka barabara nikamuuliza kwa nini hakusimama. Akasema sio lazima, sasa hapa unajenga au unabomoa? We need regulations ambazo zisipotekelezwa lazima ziwe na meno makali.

Ajali nyingi zinazotokea hazikupaswa kuwa na maafa na tunapoteza Watanzania wengi kwa uzembe.

Kuhusu shule hapo napo lazima tuwe makini, Je, tunataka shule ziote kama uyoga bila regulations? Hili linanikumbusha jinsi bureau de change zilivyokuwa nyingi Bandari salama lakini ukweli zilikuwa zinatapeli pesa za Serikali kwa kufanya biashara. Bank zilikuwa zinaota kama uyoga lakini chini ya JPM ameweka sheria kali ndio sababu exchange rate ya Tsh imetengemaa (Regulation). Sheria zetu ziwe za kufanya shughuli au biashara ziwe madhubuti zaidi.

Swala la Banks kutokuwa na foleni nafikiri ni kwa sababu ya mobile money.

Kuhusu private school ratio/walimu, kulikuwa na tatizo kubwa kwenye elimu lakini naona Serikali inaliangalia hilo kwa macho mawili. Kuna Private schools nafikiri quality yake sio sawa na kile wanacho-charge. Hili ni tatizo lakini halina njia ya haraka kulitatua. Tunahitaji walimu qualified kufundisha masomo ambayo wanayaelewa vizuri, vile vile nafikiri Serikali ijitahidi katika ukaguzi kuona kwamba walimu wanafahamu vizuri kile wanachofundisha kwa sababu ukiwa na mwalimu mbovu usitegemee kuwa na wanafunzi bora. Kwenye elimu mimi nilisha toa maoni nafikiri yamo humu JF. TZ wawe na mkakati wa kuwapeleka wanafunzi kama 500-1000 kusoma nje hasa kwenye vyuo vikuu vya UK, USA and (Canada), Germany, Japan, Sweden, China and Russia. Vile vile kukuza exchange co-operation na vyuo vya nje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…