Kiwanda cha kisasa cha dhahabu kitakavyosafisha dhahabu tani 100

diana chumbikino

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
428
Reaction score
368
KAMPUNI ya Geita Gold Refi nery Limited (GGR) inayomilikiwa na wawekezaji Watanzania inajenga kiwanda cha kisasa kuliko vyote Afrika Mashariki cha kusafisha dhahabu inayotoka kwa wachimbaji kwa kiwango cha kimataifa. Kampuni hiyo ilipewa leseni ya kusafisha dhahabu ambayo ni tayari kwa matumizi (RFL 001/2019) na Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini Julai 16, mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa na kampuni hiyo kwa gazeti hili jana na mmoja wa wakurugenzi wake, Sarah Masasi, kampuni hiyo itakuwa na uwezo wa kusafisha dhahabu inayofikia tani 100 kwa mwaka yenye ubora wa juu kabisa wa asilimia 99.99. “Uzalishaji utakuwa kwa viwango vya juu vya kimataifa vitakavyothibitishwa na mamlaka za kupima viwango. Masuala ya usimamizi wa mazingira, usalama wa wafanyakazi, yataendeshwa na kusimamiwa kwa viwango vya kimataifa,” ilisema.

Masasi alisema kiwanda hicho kitakuwa cha pili kwa ukubwa Afrika baada ya kiwanda cha aina hiyo kilichoko Afrika Kusini. Mbali na kuongeza mapato ya serikali, kufunguliwa kiwanda hicho kinachotazamiwa kutumia mabilioni ya pesa, kutaongeza nafasi za ajira na kukuza teknolojia ya kisasa itakayoongezea thamani ya madini ya dhahabu na kuongeza faida yake kwa taifa.

Juzi kampuni hiyo ilishiriki maonesho ya dhahabu yaliyofanyika kwa mara ya pili Geita na kueleza mpango wake huo mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha dhahabu ya madaraja ya juu inayotambuliwa kimataifa ya miche ya dhahabu ya kilo moja moja na ya aunzi 400. “Kiwanda pia kitakuwa na chumba cha kuhifadhia dhahabu ghafi cha kiwango cha juu kabisa duniani katika tasnia ya dhahabu,” ilisema taarifa ya kampuni hiyo.

Ilisema sehemu kubwa ya wamiliki wa kampuni hiyo ni Watanzania na wanawekeza kuunga mkono mkakati wa kitaifa wa kuelekea uchumi wa kati unaotegemea viwanda. Taarifa ilisema kampuni hiyo itadumisha ushirika wa kitaalamu na mashirika kadhaa ya kimataifa yanayohusiana na sekta ya madini. “Dhamira yetu ni kuongeza imani ya umma na ya kimataifa katika sekta ya madini ya Tanzania.

“Usafishaji wa madini utakaofanyika utadhibiti utoroshaji wa dhahabu nje ya nchi kwa kuzalisha dhahabu itakayotambulika kimataifa kwa kuwa na alama muhimu na nambari za lakiri. Pia tunatumia teknolojia inayosaidia utambuzi,” ilisema taarifa. Taarifa ilisema itawawezesha polisi na maofisa wa forodha kutambua haraka usahihi wa dhahabu iliyoidhinishwa kwa usafirishaji kama ni sahihi au siyo na pia ni rahisi kutambua dhahabu bandia.
 
ULINZI WA RASILIMALI ZA TAIFA NI KIPAUMBELE CHA SERIKALI YA AWAMU YA TANO.
 
Sarah masasi wa masasi contractor au? Kama ni uyu alipiga sana pesa kipindi cha awamu ya tatu hadi tenda ya plate number.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…