Kiwanda cha kutengeneza ndege Tanzania!

Kiwanda cha kutengeneza ndege Tanzania!

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
620
Reaction score
1,240
Hivi unajua nchini Tanzania kuna kiwanda ambacho kinahusika na kutengeneza ndege, inaitwa Airplane Africa limited ni kampuni iliyopo Mazimbu mkoa wa morogoro ambayo inamilikiwa na wawekezaji toka Jamhuri ya Czech.

Ni kampuni ambayo inajihusisha na kutengeneza ndege za kubebea Abiria kuanzia wawili mpaka wa nne. Khatibu mkuu wizara ya Uchukuzi Profesa Godius Kahyrara amesema wizara yake itaongeza nguvu juu ya kampuni hii ili kuweza kuongeza ufanisi kwenye kuunda Ndege.

Kahyrara ametembelea kiwanda hicho leo jumanne ya tarehe 7 /11/2023 kwa kuongezea kuwa mafundi wanaofanya kazi kwenye kiwanda hicho wengi wao wamesoma chuo cha Usafirishaji (NIT)..

ndege%E2%80%93%204.jpg

Hivyo ni muhimu kwa kiwanda hicho kwani kitasaidia sana kutoa Uzoefu kwa wanafunzi kutoka vyuo vikuu, vyuo vya kati na vyuo vya ufundi kuweza kujifunza mambo mengi kuhusu kutengeneza ndege nk..

Unafikiri Tanzania Inaweza kuingia kwenye soko la Ushindani kwa kuuza ndege kwenye mashirika au nchi nyingine?
 
Ndoto za alinacha na kujilisha upepo.Tanzania ipi?Wapi?Raia wapi?Kwa umuhimu upi? Uliowekezwa kwenye hiyo elimu?Kwa competence ipi ya Sayansi iliyopo Tanzania?Na toka lini Tanzania elimu ni kipaumbele namba moja especially Science field ukilinganisha na siasa na uongo uongo na utapeli?

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
 
wangeanza hata na bajaji nadhani wangekuwa wamefanya kitu,ndege[emoji53][emoji53]

hata hao airbus au boeing wenyewe wanahusisha kampuni kibao mpaka ndege yao inapaa.
 
Back
Top Bottom