Kiwanda cha mapenzi

Dr leader

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
893
Reaction score
1,021
KIWANDA CHA MAPENZI

1 Mko wapi mko wapi,mutafutao ajira
Fungeni yenu misipi, kazi ikawe imara
Na manyakanga mkupi, mje kupata amara
Ni kiwanda cha mapenzi, kimezitoa ajira

2 Kipo huko chumvini, mkoa Tanga mjini,
Mwachimba chini kwa chini, mkitafuta madini
Kazi hii ya thamani, na ghali ulimwenguni
Ni kiwanda cha mapenzi, kimezitoa ajira

3 Si rahisi wala ngumu, ila yataka nidhamu
Tabia njema zidumu, subira nguzo muhimu
Kazini uwe timamu, ujue uso fahamu
Ni kiwanda cha mapenzi, kimezitoa ajira

4 Juhudi,uvumilivu, iwe ni yako silaha
Usikose usikivu, zifiche zako karaha
Macho yatoe ukuvu, kazini uone raha
Ni kiwanda cha mapenzi, kimezitoa ajira

5 Hapa nifike tamati, natua chini kalamu
Barua ya mwenye kiti, uwahi upate zamu
Pia uwe ni banati, kesha asiwe na mume
Ni kiwanda cha mapenzi, kimezitoa ajira

©️ Abuuabdillah✍🏽
0744883353
Moshi Kilimanjaro Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…