Kiwango cha chama kimerudi juu kwasababu ya Pacome

Kiwango cha chama kimerudi juu kwasababu ya Pacome

Muite

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2013
Posts
2,971
Reaction score
6,607
Ni ukweli usiopingika kuwa kwa miaka mingi ya hivi karibuni katika ligi yetu hapa Tz ukizungumzia kiungo bora na wa kiwango cha juu lazima umtaje chama, amekuwa kwenye ubora kwa muda mrefu japo kuna kipindi ameonekana kushuka viwango hasa baada ya kurejea Simba kwa mara ya pili, vilevile amekuwa akiingia kwenye mgogoro na uongozi wa timu yake na kuleta sintofahamu.

Baada ya timu ya Yanga kumuibua Pacome ikaonekana huyu ndie kiungo anayeweza ku challenge umaarufu wa Chama, na hakina Pacome ameonyesha viwango vikubwa sana katika ligi ya Tz na ligi za kimataifa (Caf). Na kwa muda mfupi jina la Pacome limekuwa ndio habari ya mjini.

Kwa maoni yangu ni kwamba UBORA WA CHAMA UMECHANGIWA NA MAMBO MAWILI

1. Trending ya PACOME
2. Kujisafisha kwa uongozi na wanachama wa Simba kutokana na tuhuma alizokuwa anahusishwa nazo.

NB:
Inaonekana huenda tuhuma za kuihujumu klabu ilipocheza na Yanga zikawa zina ukweli mkubwa. Ninaamini hivi maana Chama aliyecheza na Yanga ni tofauti kabisa na huyu tunayemuona sasa.

Adios Amigo
 
ORODHA YA WACHEZAJI WA YANGA WALIOSHINDANISHWA NA CHAMA.

1. HARUNA NYONZIMA.
2. SAIDO NTIBAZONKIZA.
3. FEISAL SALUM.
4. AZIZI KI STEPHEN.
5. MAX NZEGELI.
6. PAKOME ZIZUUU.
7.....
8........
100..........
 
Chama huwa anacheza kwa kuamua.
(Anacheza nw mkataba)

Mkataba wake unapofika kikomo ndio huwa anakuwa vile.(anakiwasha).
Anacheza kwa kiwango cha juu sana

Ana tabia za Pogba
Morison
Na wachezaji Wengine.

Ni mchezaji mpuuzi sana
 
ORODHA YA WACHEZAJI WA YANGA WALIOSHINDANISHWA NA CHAMA.

1. HARUNA NYONZIMA.
2. SAIDO NTIBAZONKIZA.
3. FEISAL SALUM.
4. AZIZI KI STEPHEN.
5. MAX NZEGELI.
6. PAKOME ZIZUUU.
7.....
8........
100..........
nani huwa anawashindanisha, hizo ni propaganda za timu ya MOE
 
Back
Top Bottom