Nakumbuka elimu ya kujitegemea (Self Reliance). Hii ndio elimu niliyokuwa naipendaa sana kwa wakati ule. Tulifundishwa kilimo bora,
Yes,,we have KILIMO KWANZA!!
lol
.....halafu kila mwaka Waziri wa elimu na manaibu wake watakuwa wanatusomea matokeo ya mitihani......Elimu imebinafsishwa nchi hii ndugu yangu. Watasoma vizuri watoto wa walioko kwenye mikondo ya rushwa na ufisadi tu. Mitihani ya NECTA na kwingineko imeingizwa sokoni kama bidhaa nyingine yoyote. Shule za Msingi na sekondari za serikali zimetelekezwa. Hazina Walimu, hazina vitabu vya kiada na ziada, hazina madarasa, madawati watoto wanaambiwa wanunue wenyewe,,,,
Kama Kova anavyofanya na bunduki zake kwenye luninga zetu huku ujambazi unaendelea. Kila mtendaji serikalini anajitajihidi aonekane kwenye Tv na kesho yake magazeti yaandike......halafu kila mwaka Waziri wa elimu na manaibu wake watakuwa wanatusomea matokeo ya mitihani......
Kweli tumeuzwa
Ah hizi TV zetu zinawapumbaza watendaji wetu kweli kweli.Kama Kova anavyofanya na bunduki zake kwenye luninga zetu huku ujambazi unaendelea. Kila mtendaji serikalini anajitajihidi aonekane kwenye Tv na kesho yake magazeti yaandike.
Kwa hiyo kwa mfumo huu wa kuchukua walimu wasiojiweza kwenda kufundisha ni kudidimiza nchi, maana uti wa mgongo wa maendeleo ktk nchi yoyote ile ni Elimu, na si kilimo kama tunavyojidanganya.. Elimu ni kila kitu. Taifa likiwa limeelimika hata maendeleo ya Kilimo, afya, na maeneo mengine yatakuja tu kwa kasi mpya.
Ukitaka uone jinsi ambavyo uandaaji wa walimu ni mbaya fatilia vyuo vya walimu, na vyuo vikuu wakati udahili unafanyika.
Ukiulizwa, " Umeomba kozi gani?"
Ukijibu, " Ualimu! "
Basi utachekwa na utadhalauliwa sana kwa sababu zifatazo:
1: Umepotea njia (Umepoteza mwelekeo)
2: Maisha yako unayaweka pabaya maana mshahara wako baadae ni kiduchu.
3: Inaonesha umefeli sana.
Au utasikia mtu(rafiki au mzazi) anamwambia mwenzake aliekosa udahili:
"Hata ualimu(Education) umekosa???????!!, aya yaya yaa yaa duh!
"Hata ualimu!!!!!!!!!! nao umekosa "
Ualimu umedhalauliwa sana na haupewi nafasi yake kama inavyotakiwa.
Watu wengi wana talent za ualimu na ni wazuri ktk masomo. Lakini, nani aende ualimu wakati wengi wanaoenda huko ni feliaz na wanahofia mapato yao ya baadae!!.
Kwa kweli inasikitisha, inatia uchungu sana. Ila tutafika tu siku moja..