Gelange Vidunda
JF-Expert Member
- Aug 18, 2008
- 314
- 31
Tulichukua watu waliofeli tukawapa ualimu, sasa tunaona matokeo yake. Haiwezekani mtu aliyepata Div IV points 28 akamfundisha mtu akafaulu vizuri. Mara nyingi hawa utakuta hesabu na kiingereza kwao ni shida sana, hivyo wanafunzi wanatoka shule za msingi hawana msingi mzuri wa hesabu na kiingereza hivyo na huko mbele matokeo ni yale yale
Katika nchi nyingine ualimu ni kazi ya watu waliofanya vizuri kabisa katika masomo yao, na ndiyo huweza kuwafundisha vizuri wanafunzi wao kwani wanajua vyema kile wanachokifundisha.
Hapa Tanzania si ajabu kwa mwanafunzi kumuuliza mwalimu swali, nae akashindwa kujibu!
Angalia vyuo vikuu vya wenzetu, ni vituo vya utafiti na ugunduzi wa mambo mbalimbali ya kisayansi sisi hapa ni vyuo vikuu vingapi vinafanya utafiti wa kisayansi na matokeo yake yaliyotangazwa ni mangapi na yapi?
Tumeshuhudia hivi karibuni degree feki! Huyu mwanafunzi aliyefundishwa na mwalimu feki, na ikadaiwa amefaulu naye si amefaulu katika ufeki tu!.
Hatua za kuchukua:
Kuanzia sasa, watu wa kusomea ualimu kwa waliomaliza kidato cha nne, wawe wamefaulu kwa Div III. Tusilazimishe kuwa na walimu wengi ambao ni mabomu tutazidi kutumbukia shimoni.
Wanafunzi wa shule za msingi wanaofaulu hisabati, kiingereza na sayansi, wapelekwe kwenye shule za sekondari ambazo kuna uhakika wa waalimu wa kuwaendeleza. Tumeshuhudia hivi sasa wote wakipelekwa shule za kata ambazo tunakiri hazina waalimu tunawapoteza watoto hawa!. Tunaweza kwa kuanza kutenga shule moja katika kila tarafa na kuipa kipaumbele hicho waalimu wa sayansi na hisabati, na mabweni, ili kwa kila tarafa wale wanafunzi waliofaulu vizuri masomo hayo waende kwenye shule hizo
Mshahara kwa wanasayansi uwe mkubwa kuanzia kwa mwalimu anayefundisha masomo hayo ngazi yoyote ile hadi kwa wanaofanya kazi za kisayansi.
Mwanafunzi mmoja nilikuwa namhimiza asome hisabati na sayansi ili aje ashike nafasi yangu ya uhasibu, aliniuliza- hivi wewe na Meneja wako nani ana mshahara na marupurupu zaidi nilimjibu kuwa ni meneja wangu. Akaniuliza, yeye amesomea nini?
Tufike mahali wataalamu tuwape malipo mazuri, zile enzi za kusema meneja ana majukumu ya kiuongozi hivyo alipwe zaidi kuliko mtaalamu aliye chini yake, zimepitwa na wakati.
Matokeo ya mtihani wa Form II yaliyotangazwa jana ni ushahidi tosha
Ibrah said:Mwisho, ni mwaka juzi tu ndipo Rais JK alipoamua kutoa tamko la kupiga marufuku shule kutumia vitabu tofauti-tofauti vya kiada. Kabla ya hapo (sijui kama tamko limetekelezwa au la) kila shule ilikuwa inatumia kitabu chochote tu cha kiada kama Uongozi wa shule ulivyoona inafaa. Utakuta kitabu cha Jipografia cha Darasa la 5 kinachotumika na shule moja ni tofauti na kinachotumika na shule nyingine. Katika shule za English Medium hilo ni suala la kawaida hadi sasa!
Hofstede said:Nakubaliana na wewe kwa 100%. Ukweli ni kwamba mwalimu alitakiwa kuwa ni best student, yaani mtu alifaulu kwa kiwango cha juu kabisa.
Mkandara, naona unakataa kuelewa.
Mwaka 2000, 19% ya watoto waliokuwa darasa la saba walifaulu mtihani wa kuinga kidato cha kwanza. Mwaka 2005, hio asilimia ya kufaulu mtihani wa kuingia kidato cha kwanza iliongezeka ikakafika 48% . Sasa unataka kusema huko sio kuongezeka kwa ubora wa elimu?
Asilimia ya kufaulu kidato cha nne imekuwa ikiongezeka vile vile. Angalia website ya NECTA.
Augustine MOshi
Mkandara, naona unakataa kuelewa.
Mwaka 2000, 19% ya watoto waliokuwa darasa la saba walifaulu mtihani wa kuinga kidato cha kwanza. Mwaka 2005, hio asilimia ya kufaulu mtihani wa kuingia kidato cha kwanza iliongezeka ikakafika 48% . Sasa unataka kusema huko sio kuongezeka kwa ubora wa elimu?
Asilimia ya kufaulu kidato cha nne imekuwa ikiongezeka vile vile. Angalia website ya NECTA.
Augustine MOshi
naona kama unachanganya suala la increasing access to education and increasing performance. Inawezekana kabisa hao unaowana wanaenda secondary ni kwa sababu they can be accommodate in our secondary school na sio kwamba ubora umeongezeka. what I know Tanzania is one of the country which has achieved in education quantity provision, but we still suffer in education quality provision.
Elimu ya Tanzania haijashuka; imepanuka tu. Katika kupanuka huku, ziko shule nyingine ambazo hazifikii kiwango, na ziko shule nyingi zinapita sana viwango vilivyokuwepo zamani.
Hii leo, kufaulu kumeongezeka, sio kupungua. Mtoto anayemaliza kidato cha 4 katika moja ya shule 100 bora za leo ana elimu nzuri zaidi kuliko mtoto aliyemaliza kidato cha 4 katika shule 10 bora za miaka 15 iliyopita.
Watoto wanaohitimu masomo katika shule kama Mariam, Mzumbe, St. Joseph, Ilbouru, Maria Gorreti nk. wameelimika zaidi kabisa kuliko watoto waliohitimu miaka 15 ya nyuma.
Elimu ya Tanzania iko katika kipindi cha kupanda na kuongezeka kimapinduzi.
Augustine Moshi
wa kulaumiwa ni serikali kwa kutoweka sera ya elimu, ikawa ni ruksa kwa waziri au kamishina kutunga au kuelekeza atakavyo, walimu kupuuzwa, na wanafunzi wa ngazi zote kuwekwa mazingira ya ajabuKama wazee wanapima vijana kwa kipimo walichopimiwa wao then kiwango kimeshuka, kama vijana wanaopata elimu wanaona wenyewe kuwa inawasaidia then hakijashuka. Japo si mzee wala kijana najua kuwa watu wanakuwa wabinafsi zaidi kadiri siku zinavyoendelea. Asipotokea mtu wa kureverse hii (hopefully JK) tunaishia pabaya very soon. Tatizo la elimu kama lipo kwa nini halishughulikiwi? Ina maana hakuna wataalamu? Mbona kila siku wanasomeshwa? Tunasomesha wataalamu wengi sana hatutakiwi kuwa na sector isiyokuwa na wataalamu WA KUSOLVE PROBLEMS. Sio kuandika mada.Ni aibu kuzuzungumzia hili jambo miaka nenda rudi.Let us do it, find a solution and stick to it.