Nauza Kangala huku nafundisha huu mwaka wa kumi. Wateja wangu wakubwa ni walimu wenzangu. Huwa tunapiga Kangala na tunachanganya na pombe kali za bei rahisi ili kupata stimu.
Lakini tupo vizuri. Tunapiga kazi na wato wanafaulu. Ni kweli asubuhi huwa harufu inatema ila tunakuwa hatujalewa. Ni harufu tu ila ulevi unakuwa unaisha. Tukinywa maji asubuhi harufu kama perfumu ya miwa mdomoni.
Sasa ni katika hali gani ambapo mtasema temeshindwa kazi maana tunahudhuria kila siku na kazi tunafanya?
Hakuna kipimo hata uingie na konyagi sita ofisini , tatizo ni ulevi unaopelekea kushindwa kutimiza majukumu yako ..Hakuna sehemu wamekataza pombe ila ukilewa mpaka ukashindwa kutimiza majukumu au ukaleta vurugu ofisini basi habari yako kwisha.