Kiwango kikubwa cha Kansa kanda ya Ziwa kiangaliwe

Tatizo la cancer kuwa kubwa mikoa ya Kanda ya ziwa sio tatizo geni ila lipo toka miaka michache iliyopita ,serikali inalijua na Kwa kutokuwajibika wako kimyaaa muda mrefu nahisi Kuna watu wananufaika huku maelfu wanapoteza maisha... ..Hawa watafiti wa nchi za nje Mara nyingi huwa wanafanya utafiti kwa interest zao na kwa manufaa Yao..either wakwepeshe tatizo au wabuni bidhaa wafanye biashara.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mungu wabariki Wazungu
 
Turudie labda kusema kwamba hii story ya mlipuko wa cancer kanda ya ziwa ni njia iliyozoeleka ya ubeberu kuendelea kuitawala dunia kwa kwa kujifanya wao wana data zote duniani, wana maarifa yote duniani, na wana umuhimu wa kipekee kwa kutoa taarifa ambazo zina maslahi kwa watu wa kawaida wa nchi husika.

Ndio maana watoto wetu na vizazi vyetu vijavyo tunavifundisha critical thinking. Critical thinking ni uwezo wa kutathmini habari au taarifa, ya kusimuliwa au kuandikwa. Ukiwa na huo uwezo wa critical thinking unaweza kutanabaisha nini ukweli, nini uongo, nini kinaendelea nyuma ya pazia.

Suala la ongezeko la cancer duniani ni suala ambalo hauwezi hata siku moja kulitengea story ya kijiogrofia eti great lakes. Cancer ni ugonjwa ulioongezeka sana duniani kutokana na mambo mengi mtambuka: huko kwa wazungu kuna cancer nyingi sana kuliko hata Afrika. Kitendo cha kusingle out great lakes za east africa kina agenda nyuma yake, na kama ukienda Bugando utakuta wagonjwa wengi wa cancer wanatoka ukanda wa ziwa sababu Bugando ipo Mwanza. Ni sawa na kusema Dar wanapata sana ajali za pikipiki kwa sababu Muhimbili ina idadi kubwa ya majeruhi wa idadi ya pikipiki. Again, watanzania tujifunze kuchukua habari za wazungu wanazoteport kuhusu sisi kwa jicho la tatu
 
Ninachokiona rate ya upimaji wa saratani iko chini ndio maana saratani iko juu.
 

OSHA wanachokijua ni kwenda kwenye maofisi kufanya inspection na kupeleka invoice kubwa kwa aliyefanyiwa inspection.
Issue km hii ambayo ni life threatening wako nyuma kabisa.
Wanakimbizana na makusanyo tu hawa jamaa.
 
Resources is a curse and not blessing.
 


Unasema ubepari wakati Magufuli alishasema hili na waziri wa Afya. Hizi ni data za Tanzania sio za UN au USA!. Kuna vitu ambavyo sio vya kulaumu wengine mfano data zinaoneonyesha cancer zimeongezeka badala ya kutafuta sababu na kuokoa maisha tunazungumzia data za wenzetu! sasa hata kama ni kweli kwamba cancer huko US ni zaidi yetu ina maana sisi tusijali ongezeko wa wagojwa wengi tena wa kanda moja tu!. Kwenye haya mambo tuweke siasa pembeni na kujaribu kuokoa maisha ya wananchi.

Kama hujui US pekee wanasaidia $600M kwenye Afya sasa kama wangetaka tufe kwanini watume pesa za kujenga hospitali na kufanya chanjo kwa watoto wetu.
 
So then US wakikupatia USD 600 M kwa ajili ya kusupport afya una uhakika gani kwamba hiyo ni aslimia ndogo sana ya wanachobeba kwa mkono wa pili kupitia mikataba kibao inayofavour makampuni ya kimarekani?

Na ni lini nyie watu mtaacha kutumia misaada ya fedha za marekani kama fimbo "smoke-screen" ya kupenyeza pro-American agenda? Embu mtwache kwanza, na huo ukoloni mamboleo wa kuiona Marekani kama lidude flani lenye sifa za kiungu ndicho wenzenu wanachokitaka wakati mna uwezo nyie wenyewe wa kujipangia vipaumbele vyenu.

Na tunaporudi kwenye cancer hii iliyoreportiwa na "wamarekani" mimi sijasema kwamba hatuna sababu ya kuchunguza au kujitafutia uwezo wa kukabiliana na magonjwa ya cancer hapa Tanzania. Sema nipo kinyume na hizi overhypes kwa mmarekani. Sasa kumbe kama hata Magufuli na wizara ya afya washawahi kulipazia sauti then hakukuwa na hata sababu ya kuwaingiza wamarekani kwenye hii stori.
 
Na hapo juu nimesahau kukwambia jinsi ambavyo pesa yoyote anayoitoa mmarekani ni kwa ajili ya interest za Marekani kwanza kabla ya interest zako. Na kwa bahati nzuri sana kwao tayari wameshatangulia sana kiasi kwamba akikupa wewe 600M kwenye afya ambayo hiyo hela utaitumia kununua dawa mbalimbali wanazoziuza wao, yeah kwa upande wenu wapewa msaada mtajiona mmefaidika (mmepata dawa) but obviously pharma industry za marekani zilizotapakaa dunia nzima keep on running. Na labda niliweke hili vizuri: mi sipo kinyume na Marekani na interest zake, after all ni wajibu wa kila nchi kushinda mechi zake. Kitu ambacho niko kinyume nacho kabisa ni hizi western propaganda machine zinazotaka jambo fulani nyuma ya pazia kwa njia ya hila na udanganyifu. Watajifanya kuhubiri uhuru na demokrasia kumbe wanachokitaka ni nchi za dunia hii kuwa na mazingira wezeshi kwa ajili ya biashara zao, watajifanya kuhubiri soko huria kwa sababu viwanda vyao tayari vina uwezo wa kuzalisha bidhaa mbalimbali kwa unafuu zaidi hivyo zinaweza kushindana sokoni kuliko zenu nyie mnaoanza. Kila wanachofanya kina agenda nyuma yake.

Wangekuwa direct kama mchina anavyokuja, tupe hiki tuwape hiki nisingekuwa na shida nao kabisa.
 


Inawezekana hujui mimi nipo US kwa miaka 25 sasa.Pili mimi nafanya kazi kwenye kampuni za mikataba ya madawa hapa Marekani kwa zaidi ya miaka 10. Huo unao ongea ni uvumi hauna ukweli wowote ni maneno ya vijiweni. Nenda kasome vizuri maelekezo ya hiyo pesa halafu uje na uhalisia ni dawa zipi za US wanaenda kununua. MSD wana nunua dawa za generic kutoka India sio US.
 
Ni dawa zipi tunazonunua kutoka Marekani na zina thamani gani. Naijua kiasi flani sekta ya afya, utakaponijibu andika ukweli
 
So? Mtu kama wewe unayefaidika moja kwa moja kwa maslahi ya marekani utasema chochote tofauti na script ya unayemtumikia? MSD inanunua dawa generic lakini pia inanunua prescription drugs. Na wala sisemi kwamba $600m lazima zote zirudi kwa aliyezitoa. Ninachosema ni kwamba hawatoi hizo 600m kama free lunch, watakupa 600m lakini wana lengo na namna ya kupata faida zaidi ya hizo walizozitoa. Na wamejenga mifumo sophisticated soft and hard kuhakikisha kwamba maslahi yao yanalindwa.
 
Ni dawa zipi tunazonunua kutoka Marekani na zina thamani gani. Naijua kiasi flani sekta ya afya, utakaponijibu andika ukweli
Hata sijaelewa lengo la swali hili sababu wewe unaijua sekta ya afya lakini mimi pia nina ka ufahamu kuhusu life cycle ya drugs na jinsi hizi biashara za dawa zinavyooperate. Pharma companies zinazotengeneza madawa yote maarufu nyingi zinamilikiwa na Marekani hata zile zilizo Ulaya (mfano Novartis). India ndio wanatengeneza madawa mengi under generic licence lakini lazima wanunue authorization kutoka kwa original manufacturers.
 


MSD inanunua dawa generic lakini pia inanunua prescription drugs

Nikueleweshe kidogo prescription drugs sio aina ya dawa ni dawa yoyote ambayo inahitaji Dr akuandikie ndiyo uweze kununua.
2014 MSD walitaka kunipa kazi kama Director wa supply chain na niliongea na mkurugenzi mkuu ndiye aliyesema kwa uhakika wana nunua dawa ambazo ni generic kutoka India. Kuna Brand na Generic inawezekana ndiyo ulivyotaka kusema lakini Brand drug nyingi hata sio za kampuni za USA.

Tujitahidi kuongea ukweli sio uzushi ambao hauwasaidii watu.

Jiulize Wewe binafsi unafanya nini kupunguza mpasuko wa cancer kanda ya ziwa. Mimi hapa natoa elimu na kutangaza je wewe unafanya nini?
 
Mna uhakika kuna mpasuko mkubwa wa Cancer kanda ya ziwa??
Yaah mkuu ni kweli, mimi nathibitisha hili sababu nafanya kazi taasisi ya saratani Tanzania lakini sio daktari.
 
Kansa kanda ya ziwa TZ ni kipengele mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…