Kiwanja cha meter 11x15 naweza jenga vyumba 3 na sehemu ya Parking?

Wakuu Kama kichwa kilivotanabaisha hapo juu,Kuna mahali nina kaplot ka ukubwa wa Meter 11x15 nataka nianze kukafanyia kazi.je naweza fyatua kanyumba ka chumba tatu na eneo la parking likabaki?
Labda kwa biashara, ila kwa makazi utakosa freedom, utakosa sehemy ya kupanda miti ya kivuli kwakuwa nyumba ya kawaida angalau uwe na 12x20 msq
 
nikiwa kwa kitanda peni na karatasi uwa havikosekani karibu yangu, na hii ndo wazo langu la haraka baada ya kuona hili bandiko. mchoro rahisi lkn wenye faragha kulingana na ukubwa wa kiwanja ambacho ni 11x15m. note: sijazingatia location ya kiwanja sbb sikijui

 
Good try but dinning ya mita mbili ni ndogo sana. Nyumba ndogo huwa haziwekwi dinning.
 
Wee jamaa ni mkali wa hizi kazi.
 
Inawezekana mkuu, with open concept floor...

Cha muhimu labda pia uweke bayana mahali ulipo pako vipi (tambarare au mwinukoni)?

Ushauri, kama ni tambarare unaweza jenga kwa L shaped, kama ni mteremkoni na pesa inaruhusu unaweza jenga semi double floor
 
This is okay....ondoa partition kati ya sitting na dining baaasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…