Kiwanja cha ndege Chato

ngalanga

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2015
Posts
1,782
Reaction score
1,887
Poleni kwa majukumu wakuu.

Kiroho safi naomba niende kwenye kichwa cha habari ambapo ningependa kuuliza kwa ambaye ana takwimu sahihi kuhusu kiasi cha ndege zinazotua uwanja wa Chato iwe per day au per week nk.

Nauliza kwa nia njema kabisa kwavile ningependa kujiwekeza huko katika sekta ya Utalii.

Karibuni wakuu
 
Bado hakijafunguliwa, subiri kifunguliwe kwanza ndio utapata jibu la swali lako
 
Acha uongo huo mbona ndege zinatua mpaka marais wa inchi za nje tayari wametua hapo au una maanisha bado hawajafanya show ?
Bado hakijafunguliwa/hakijazinduliwa.

Ulishawahi kusikia au kuona ATCL inafanya safari za Chato kama safari za Mwanza, Dodoma, Songwe, Kilimanjaro?
 
Bado hakijafunguliwa/hakijazinduliwa.

Ulishawahi kusikia au kuona ATCL inafanya safari za Chato kama safari za Mwanza, Dodoma, Songwe, Kilimanjaro?

ATCL siku hizi sio siri kwani wanaenda Chato mara kwa mara ingawa sio kila siku kama mfano wako uliotaja lakini kama unazungumzia safari za ATCL za Chato za kibiashara hapo sina uhakika kama hilo linafanyika au laa
 
Habari wana jamvi, kwa muda nimekuwa nikisikia kuna uwanja wa kimataifa uitwao Chato International Airport. Binafsi siujui, lakini sijawahi kuona uzinduzi wake, vilevile sijaona hata kwa vyombo vya habari kuhusu ndege zinazotua kwenye huo uwanja.

Mwenye takwimu anijuze huu uwanja ukoje na kwa siku unapokea wastani wa ndege ngapi. Lakini nilitaka kujua kama tayari Bombadier za ATCL zinatua kwenye uwanja huo
 
TCAA na TAA karibuni sana hapa JF kwa ufafanuzi na takwimu sahihi.
 
Hivi kwa nini huu uwanja haufanyiwi uzinduzi rasmi kama miradi mingine ya serikali ya awamu ya 5 ya Mh. Dr. Magufuli?
 
Mkuu kuwa mpole, Jitahidi uangalia TBC, siku wakizindua wataweka data hizo zote.
 
Paundwe jopo la Maprofesa wakafungue University of Chato
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…