Kiwanja cha shule iliyoanza miaka 40 iliyopita, Ngara chatwaliwa.

Kiwanja cha shule iliyoanza miaka 40 iliyopita, Ngara chatwaliwa.

ngarawatch

Member
Joined
Jun 26, 2024
Posts
24
Reaction score
14
Baraza za Ardhi na Nyumba limetoa amri ya kuchukuliwa kiwanja cha michezo na mapumziko cha Shule ya msingi Mukirehe iliyoko wilayani Ngara.

Kufuatia uamuzi huo, aliyeshinda kwenye shauri hilo, amejenga uzio kuzuia wanafunzi kutumia kiwanja cha shule hiyo iliuyanza zaidi ya miaka 40 iliyopita.

Mmiliki wa sasa wa eneo hilo anayetajwa kwa jina la Leah Semuguruka, kupitia kampuni ya udalali ya Shushana Services Co Ltd , 21/02/2024, kwenda kwa serikali ya kijiji cha Mukirehe kukabidhi eneo hilo.

Makala ya barua hiyo imenukuliwa kwa OCD wa wilaya ya Ngara, ilitaka eneo hilo kukabidhiwa ndani ya siku 14 tangu tarehe ya kutolewa kwa barua hiyo.

Uongozi wa wilaya ya Ngara kama kawaida wanashughulikia masuala muhimu zaodi ikiwa ni pamoja na siasa za kuelekea uchaguzi mkuu ambapo majina makubwa yanatajwa kulitaka jimbo hilo kutoka kwa mbunge wa sasa Ndayisaba Ruhoro.
 
utawala wa sheria ukiwepo, hata ikulu inaweza kuchukuliwa, ama la, wampe kingine au wampore na wampe compensation inayotosha/yakuridhisha. hiyo ndio haki.
 
utawala wa sheria ukiwepo, hata ikulu inaweza kuchukuliwa, ama la, wampe kingine au wampore na wampe compensation inayotosha/yakuridhisha. hiyo ndio haki.
Ndugu.
Wakati mwingine huo unaoitwa utawala wa sheria hutumiwa na wajanja kupindisha maamuzi ili kupendelea upande mwingine.

Tatizo hapa ni uongozi wa wilaya kukaa kimya kana kwamba hakuna kilichotokea.
 
Pambana, Bro wadogo zako wapate tena kiwanja chao ili wajenge afya, kukuza vipaji na kujenga urafiki.

Waambie viongozi wako wachukue hatua
Siko Ngara Kwa Sasa mkuu.
Ila nitarejea hakika
 
Huyo mama naye ana roho mbaya. Angeomba eneo lingine kufidiwa.
La atoe sadaka kwa serikali, ni eneo la shule....angejivunia thawabu hata baada ya kufa kwake.
 
Shule iko hapo tangu miaka 40 iliyopita

Hili jambo mbona lina ukakasi sana

Ni cha kwake au cha urithi?

Imetumika haki au rushwa?
 
Huyo mama naye ana roho mbaya. Angeomba eneo lingine kufidiwa.
La atoe sadaka kwa serikali, ni eneo la shule....angejivunia thawabu hata baada ya kufa kwake.
Serikali which?

Tatizo serikali haitendi haki.
 
Mkuu, kwani serikali ni nani?
Angelitoa eneo kwa kijiji litumike kama eneo la shule ndio hiyo hiyo serikali.
Wacha serikali inunue tu. Inachukua Kodi afu wanatumia kwenye starehe tu.

Serikali ni watu wachache wanao zani kwamba wanatawala watu wote.

Kusema serikali ni watu ama Kijiji ni zilipendwa.
 
Back
Top Bottom