Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Niliwahi kumtembelea rafiki yangu, alipewa sehemu ya kujenga nyumba na wazazi wake, eneo halikua kubwa sana lakini ni katikati ya mji.
Alijenga ghorofa na juu aliweka vyumba viwili vya kulala. Ngazi za kwenda vyumbani zilikua za design hii hapa kwenye picha. Choo na bafu vilikua chini pamoja na sebule na jiko.
Nilikaa weekend nzima, usiku ukitaka kutumia choo inabidi ushuke ngazi. Nilimuuliza furniture walipandishaje juu. Aliniamia vitanda na makabati ilibidi viungwe huko huko vyumbani. Fundi serumala alikuja na chaga, na matendegu, milango ya kabati nk.