Habarini,
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo Juu, kuna ndugu yangu anauza kiwanja chake kilichoko maeneo ya Mbutu Kichangani, kimepimwa kikiwa ni Mojawapo ya Viwanja zaidi ya 30 vilivyopimwa na Kampuni ya Makazi Solutions kwa Kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.
Kwanja hiki kina eneo la SQM 650, na kiko kilometa 29 kutoka Ferry, ikiwa ni Kilometa 24 kuanzia Ferry mpaka Dege yalipo majengo mapya ya NSSF yanayojengwa sasa (
MPENJA BLOG: WAJUMBE BODI YA WAKURUGENZI NSSF WATEMBELEA UJENZI MRADI WA ‘DEGE ECO VILLAGE'), kisha unakata kushoto kuelekea upande wa baharini Kilometa 5.
Kuanzia Ferry mpaka Majengo haya ya NSSF (DEGE) ni Lami tupu, na kuanzia hapo Dege mpaka Mbutu Kichangani ni Barabara ya Kuchonga. Viwanja hivi haviko mbali sana bahari, ingawa anasema hakuwahi kupima umbali wa kuelekea baharini lakini wenyeji wanasema ni kama kilometa 2 hivi.
Umeme umeshafika mpaka NSSF kwa sasa, na mipango ipo ya kuupeleka Mbutu.
Anakiuza sababu anataka kumalizia Ujenzi katika Nyumba ingine, hivyo kuliko kua na Viwanja viwili visivyokaliwa, bora kua na Kimoja kinachokaliwa.
Kwa anetaka kukiona, basi namba ya Mwenyeji alieko kule ni 0712 080 241, Bwana Shija na anapatikana karibia siku zote hivyo ni kuweka appointment tu.
Bei ya Kiwanja hiki ni
Tshs 12,000/= kwa kila SQM 1, hivyo kwa Kiwanja chote ni
Tshs 7,800,000/= na
mazungumzo yapo.
Nimewasilisha!!