Plot4Sale Kiwanja kinauzwa Mbopo Madale

kyanyangwe

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2018
Posts
1,275
Reaction score
3,316
Kiwanja kinapatikana eneo la mbopo-madale ndani ya wilaya ya kinondoni mkoa wa Dar es Salaam.
Kiwanja hakijapimwa,ila kina hati ya mauziano kutoka serikali za mitaa.
Kiwanja kiko eneo zuri lililojengeka na linalofaa kwa makazi.
Kiwanja kimezungukwa na huduma muhimu kama maji,umeme,shule na hospital.
Ukubwa wa kiwanja ni 550sqm.
Bei ya kiwanja ni shilingi za kitanzania 8.5m
Kwa mawasiliano zaidi na ukitaka kukitembelea kiwanja piga 0734079737.
Hakuna udalali.
Karibuni sana

 
Vp bado kipo?
 
Vp bado kipo?
Ndugu kama umenunua pole lakini kama hujanunua basi mshukuru Mungu. Sasa hivi huko kuna mtafaruku mkubwa sana kwani kuna sehemu ya Mbopo DDC wanasema ni eneo lao lakini wakiombwa vielelezo hawana. Matokeo yake wahuni wameshaanza kupora maeneo ya wazi yaliyopakana na msitu wa Pande na kugawa viwanja 20x20 na kuwauzia watu wengine. Serikali ijiandae baada kutatua mgogoro mkubwa kwani waliporwa maeneo yao na walionunua shughuli itakuwa pevu muda sio mrefu. Nina ndugu yangu huko analia kwani hakuna msada wowote wala tamko la serikali na mbaya zaidi ni kama vile serikali ya mtaa inashirikiana na hao watu wanaopora maeneo ya watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…