Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu wewe toa ofa yako tuu kwenye mazungumzo hakuna linaloshindikanaa.Bei mkuu, weka bei kwanza ili mtu ajue next step!
Kiwanja chenye ukubwa wa 6000sqm kinauzwa maeneo ya Wazo Hill karibu kabisa na shule ya Wazo Hill High School. Kina Offer letter.
Ni eneo linalofaa kujenga shule, business complex, nk.
Kama unahitaji piga simu 0754 30 98 32
Mkuu wewe toa ofa yako tuu kwenye mazungumzo hakuna linaloshindikanaa.
Ni kweli matapeli wa viwanja wapo lakini kiwanja hiki ni halali kabisaa.Kwa taarifa yenu kuna matapeli wanaohaha kutafuta walio wajinga ili watapeliwe viwanja vya Wazo Hill. Baadhi ya viwanja navijua. matapeli hao wameweka chain na wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi lakini viwanja vina mgogoro ambao bado kutatuliwa. Wenye viwanja wamebana tu, lakini matapeli yanaenda kuchinja kuku na kumwaga damu halafu wanaenda na kaniki mpya nyeusi na unga. Wamechomewa vitu vyao sio mara moja na wanalialia hivi sasa.
Ni mjinga tu atakayeliwa. nenda kanunue kichwa kichwa halafu uliwe kweupe mchana. Hati wamezichora kwa vipimo vya mezani, ukienda kwenye eneo vipimo vyao haviendani na hali halisi. Watakuendesha puta ununue haraka. Jiandae kwenda mahakamani ukishanunua na kuanza kujenga. Wenye viwanja halali wanapanga wakuangalie umalize nyumba yako halafu ubomolewe kama huelewi, maana wenye akili wamekwenda wakaambiwa ukweli wameshituka na kukimbia.
Usirogwe kununua kiwanja pasipo uhakiki. Mafaili yenye viwanja vilivyo na mgogoro ambavyo waanaouza wamepata offer kiujanja na wakashitukiwa yako ngazi mbalimbali za uchunguzi.
Mwenye masikio na asikie. Madalali wanasuka mipango na maafisa wa zamani wa Ardhi ambao walishatimuliwa vyeo kwa sababu ya ufisadi huo huo. Wengi wanajulikana wazi kwa majina na wanakoishi.
Kama huyo muuzaji ana kiwanja halali na ataje namba ya kiwanja halafu ni PM. Nina wasiwasi na kiwanja kinachofanana na sq m hizo ambacho detail zake ninazo.
Mkuu wewe toa ofa yako tuu kwenye mazungumzo hakuna linaloshindikanaa.