Kwa taarifa yenu kuna matapeli wanaohaha kutafuta walio wajinga ili watapeliwe viwanja vya Wazo Hill. Baadhi ya viwanja navijua. matapeli hao wameweka chain na wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi lakini viwanja vina mgogoro ambao bado kutatuliwa. Wenye viwanja wamebana tu, lakini matapeli yanaenda kuchinja kuku na kumwaga damu halafu wanaenda na kaniki mpya nyeusi na unga. Wamechomewa vitu vyao sio mara moja na wanalialia hivi sasa.
Ni mjinga tu atakayeliwa. nenda kanunue kichwa kichwa halafu uliwe kweupe mchana. Hati wamezichora kwa vipimo vya mezani, ukienda kwenye eneo vipimo vyao haviendani na hali halisi. Watakuendesha puta ununue haraka. Jiandae kwenda mahakamani ukishanunua na kuanza kujenga. Wenye viwanja halali wanapanga wakuangalie umalize nyumba yako halafu ubomolewe kama huelewi, maana wenye akili wamekwenda wakaambiwa ukweli wameshituka na kukimbia.
Usirogwe kununua kiwanja pasipo uhakiki. Mafaili yenye viwanja vilivyo na mgogoro ambavyo waanaouza wamepata offer kiujanja na wakashitukiwa yako ngazi mbalimbali za uchunguzi.
Mwenye masikio na asikie. Madalali wanasuka mipango na maafisa wa zamani wa Ardhi ambao walishatimuliwa vyeo kwa sababu ya ufisadi huo huo. Wengi wanajulikana wazi kwa majina na wanakoishi.
Kama huyo muuzaji ana kiwanja halali na ataje namba ya kiwanja halafu ni PM. Nina wasiwasi na kiwanja kinachofanana na sq m hizo ambacho detail zake ninazo.