Kuna taratibu ambazo wakati mwingine zinakiukwa kwa sababu ya udhaifu wa watawala ktk eneo husika, kwa mfano unaponunua shamba lililo kando ya mto, kuna umbali wa kuacha toka kingo za mto mpaka shambani kwako, kutoka mwisho wa maji ya bahari kuna uwazi ambao ni lazima uachwe mpaka linapoanzia eneo la kujenga cho chote, hivyo hivyo ktk pwani za ziwa.
Ni juu ya wewe mnunuzi kuuliza kanuni hii kwa wahusika, watakapokuja watawala wanaomaanisha, unajikuta unapata hasara kubwa kama ilivyo kwa Dsm kwa sasa. Kwa hiyo viwanja vya karibu na beach, au karibu na barabara kuu,milimani,mabondeni au maeneo ya umma, tununue baada ya kuziona sheria mama za mipango miji za eneo husika.