kiwewe cha waziri Mkuchika


Kigarama,

Labda hilo la CNN lakini hiyo Mao nafikiri alichosema ni sahihi hasa kama alikuwa anaongea.

Kama ni professional paper basi hapo ndio lazima kila neno liwe kama lilivyokuwa mwanzoni lakini kwenye mazungumzo ya jukwaani wala sio lazima sana.
 

Plus he owns 15 ranches in 7 states(approximately 2 million acres)...
 

MgonjwaUkimwi, don't dance around with words na kujaribu kupotosha maana. Kumiliki si neno la kufikirika hata kidogo. Kumiliki ni neno halisi na liko kwenye misamiati, kanuni, sheria, historia na mengineyo mengi katika lugha. Maneno kama utapeli, madongo, mipasho, ki-papai, n.k. ndiyo unaweza kusema ni maneno ya kufikirika. Hata hivyo hayo mengine tayari yanaingia kwenye misamiati, sheria, kanuni n.k. katika lugha.

Umiliki ni Ownership (kwa lugha ya wenzetu) na siyo kuwa na influence. Ownership is not synonymous to Influence, and vice versa.

Kuwa na influence katika suala lo lote hakukupi 'umiliki' wa hicho kitu. CCM ina influence katika maisha ya wa-Tanzania wengi haina maana kuwa inawamiliki wa-Tanzania wengi.

Tukirudi kwenye kauli za Mkuchika, nakubaliana nawe kuwa si sawa ku-split the hair katika kauli za viongozi ili kuona makosa yao. Ila kama kauli anaitoa kama njia ya kuendeleza policy au kuleta sera mpya, basi ni halali kuzipa uzito kauli na maana ya kauli hizo.
Kama ambavyo alivyosema Mkuchika "No investigation, No Right to Speak", iwe hivyo hivyo pia kwake na wenzake ""No investigation, No Right to Speak".

Part of what he said could have been proved right or wrong if he had just done that.
 

I believe you Mwafrika...
You are my favorite jamboforums person...
 
Sielewi hivi kunamjadala gani hapa!!!!!!!!!!.
mwongozo wa JF .Niupitie kidogo
 
Vuta pumzi mkuu utajua kinachoendelea!

Ahaa nimevuta pumzi mwongozo nimeupitia!!!! na nilichojitahidi kudodosa ktk maada hii kwangu naona mambo haya-

1. Hawa viongozi wetu wawe wabunifu sio kila kitu wanapiga DESA ,hata kama marekani wanamiliki hiyo CNN si lazima na sisi tuige "Ukiiga kwa tembo kunya mavi makubwa utapusuka....."

Na kutumia misemo pia nayo nafikiri inaenda na wakati na mahala si kila msemo unajenga mfano-

"Fisadi aliye juu tumpadilie huko juu kwa juu mpaka kieleweke"
Maana ukimsubiri fisadi chini TWAFA.

ILa kuhusu HEKAYA za huyo waziri alikua sahihi 10/10.
 

kama unaanzisha mhadala ni vizuri ukiachia wengine kuuhadili kwanza na ndipo kama inawezekana kutolea maelezo.

Mimi nadhani kwanza nilijikita zaidi katika mantiki ya Mkuchika kusema aliyoyasema.kwa maneno yake mwenyewe na kwa muonekano wa vitendo vya mwili wake alionekana anaashiria kwamba wale wote wenye hoja ya kusema kwamba serikali kumiliki vyombo vya habari ni makosa basi wamechanganyikiwa

na katika kuweka nyama kwenye hoja yake hiyo ndiyo akasema kwamba CNN inamilikiwa na serikali ya marekani jambo ambalo wengi wetu humu wamekubali kwamba siyo kweli

Mkuchika ni kiongozi wa nyanja ya habari hapa Tanzania na kwa kutokujua hata mambo madogo kama haya ni kuonyesha kwamba tunaye kiongozi asiyeijua vizuri njia tunaytakiwa kuipita

Ni rahisi kutokumwamini daktari ambaye atasema kwamba kipindupindu kinasababishwa na kuumwa na mbu,kama yeye hajui CNN inamilikiwa na nani atawezaje kupanga sera bora za kuendesha vyombo vya habari tanzania?

Investigation ni uchunguzi ambao hufanywa kutafuta ukweli ambao hatimaye unaweza kutoa hukumu au kusababisha kupatikana kwa mhalifu au mtuhumiwa,wakati Research ni utafiti unaofanywa kuthibitisha mantiki za nadhari mbalimbali

ama kwa kiswahili ingekuwa "kama hujafanya uchunguzi huna haki ya kusema" au "kama hujafanya utafiti huna haki ya kusema"
 
Hivi haya yoye aliyasema ili kuhalalisha kuwepo kwa CCM ndani TBC ? Si watangaze kabisa kwamba ni mali ya CCM na watumie kodi yetu kuiendesha ? Maana mambo mengine they do openly why not hili ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…